ASKOFU ALITAKA TAIFA LA TANZANIA KUTOJIBU VITA YA
MASHAMBULIZI YA AINA YOYOTE ILE
TAIFA la Tanzania
pamoja na watu wake wameaswa kuachana na
tabia ya kulipizana kisasi cha aina yoyote ile badala yake lihakikishe kuwa
linalipa ubaya kwa wema hali ambayo itaweza
kuwanyanya watanzania dhidi ya machafuko mbalimbali yanayoendelea ndani
na nje.
Kauli hiyo imetolewa Mjini Arusha mapema jana na askofu wa kanisa Katoliki Jimbo la
Arusha,baba askofu Josephat Lobulu wakati akiongea na vyombo mbalimbali vya
habari kuhusiana na maazimisho ya miaka 50 ya kanisa hilo yanayoendelea mjini hapa
Askofu huyo alisema kuwa kwa sasa Nchi ya Tanzania imekumbwa na machafuko mengi sana lakini si jambo jema kama
wananchi au taifa litaachia amani na
kisha kuingia kwenye malumbano ambayo wakati mwingine yanasababisha maafa hata
kwa wasio kuwa na hatia
Alifafanua kuwa kamwe jambo baya haliwezi kuisha kwenye
jamii kama litalipzwa kwa ubaya bali jambo baya litaweza kuisha endapo kama litalipzwa zaidi kwa wema huku wema huo ukiwa ni
viashiria vya amani ambayo wakati mwingine inapotea kutokana na ubaya ambao umo
kwenye jamii
“kama nchi ya Tanzania tutataka kupoteza amani basi tuanze
kuyafuta na kutafuta vyanzo vya vitu mbalimbali ambavyo vimezaa maovu ni wazi
kuwa damu za watu wasiokuwa na hatia zitamwagika bure sasa mimi nawasihi sana
watanzania wahakikishe kuwa wanalinda amani yao na wasiwe chanzo cha kuharibu
amani ya taifa lao”aliongeza Askofu Lobulu
Akiongelea Sekta za
elimu na afya ambazo zimo chini ya kanisa hilo
alisema kuwa mpaka sasa kanisa hilo
hususani kwa mkoa wa Arusha limeshaweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa
wanatoa elimu kwa watanzania ambapo elimu hiyo pia itaweeza kupambana na adui
Ujinga pamoja na adui Umaskini
Aliongeza kuwa kwa kuwa na sekta nzuri ya elimu ambayo
itaweza kuwaruhusu watanzania kujipatia elimu pia kutaweza kuraisisha maisha ya
vijana wa kitanzania ambapo kama watakuwa na
elimu ya kutosha basi wataweza kukimbia hata maasi ya Taifa ambayo wakati
mwingine yanatokea kwa kuwa hakuna kazi za kufanya
“tumedhamiria kuwa kwa sasa tunataka tuwe na elimu ya juu
lakini pia hata kuweza kuiboresha zaidi ambapo itatoa fursa kwa vijana wengi
zaidi lakini pia tutaweza kufikia malengo yetu ambayo tumejiwekea ya kutaka
kuwafanya vijana wa kitanzania kuwa na elimu kama
zilivyo nchi nyingine “alibainisha Askofu Lobulu
MWISHO
No comments:
Post a Comment