ASKOFU SIXBERT ATANGAZA KURUDISHA AMANI YA ARUSHA
Na Bety Alex,Arusha
KANISA la Victorius
Church Hema ya Ukombozi Sakina limetangaza kuwa kwa sasa ndani ya Mji
wa Arusha hakutakuwa na maasi mbalimbali ikiwa ni pamoja na vita ambavyo vinasababishwa na
mambo mbalimbali na badala yake historia
mbaya ya mji wa Arusha itafutika na historia ya amani itaaanza kujiandika
yenyewe
Akiongea na “nyakati”mara baada ya kuwekwa wakfu na
kuzinduliwa kwa kanisa na hema hilo
jipya lililopo maeneo ya Sakina askofu wa kanisa hilo Sixbert Paul alisema kuwa
ameingia rasmi ndani ya mji wa Arusha hivyo
ni lazima mabadiliko yaanze kuonekana
Askofu huyo alidai kuwa amepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka
na nge hivyo ni lazima mji uweze kurudisha heshima yake ambayo ulikuwa umepewa
ikiwa ni pamoja na kupunguza na kuondoa
idadi ya maovu ambayo yanatokea zaidi katika mji wa Arusha
Alifafanua kuwa kupitia madhabahu yake ni lazima uponyaji tena
wa hali ya juu sana uweze kutembea na pia uweze kuokoa watu ili lengo lake halisi
liweze kufikiwa na faida za madhabahu yake ziweze kiutumika hata na viongozi wa
kila aina huku hali hiyo pia ikichangia uwezo wa kumrudishia Mungu sifa na
utukufu
“nimekuja Arusha rasmi sasa ni lazima kila roho ambayo iko
kinyume na mapenzi ya Mungu iweze kusalimu amri na kuondoka nataka historia
mpya kwenye maisha ya kila mtanzania wa Arusha.kwa hiyo watu waanze kujiandaa
kwa uponyaji na amani ya mkoa wa huu”aliongeza
Askofu huyo
Pia alisema kuwa kupitia madhabahu yake ni Lazima hata hali
ya maisha ya wakazi wa mji wa Arusha iweze kubadilika tena kwa kiwango cha hali
ya juu sana na kila mtanzania kuwa na maisha yenye ubora na uhakika wa kiwango
cha hali ya juu kwa kuwa madhabahu yake inatenda.
“kazi kubwa ya madhabahu hii ni kufungua watu katika shida
na kisha kuwaweka huru hivyo kama watawekwa huru ni raisi sana kwao kuhakikisha
kuwa wanakula mema ya nchi yaani maisha yao yawe na ubora wa hali ya juu na
kuachana na maisha ya shida ambayo yana mwanzo na pia yana mwisho”alisema
Hataivyo wakristo mbalimbali ambao walihudhuria uzinduzi huo
walisema kuwa wanaratarajia kuona mabadiliko makubwa sana
ambayo yatasababishwa na hema hilo kwa kuwa hapo
awali Arusha ilikuwa na Vita kubwa sana
ya kisiasa hali ambayo ilipoteza maana halisi ya Arusha na hivyo kusababisha
umaskini mkubwa kwa baadhi ya watu wakiwemo wafanyabiashara.
MWISHO
No comments:
Post a Comment