CHUO CHA UFUNDI ARUSHA CHAANZA MKAKATI WA KUFUA MITAMBO YA UMEME
Chuo cha
Ufundi Arusha kimeanza mkakati wa kufufua mitambo ya kuzalishia umeme wa maji wa
Kituo cha Kikuletwa iliyopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro ambapo hadi
itakapokamilika itaweza kutosheleza mahitaji ya mikoa ya Kilimanjaro na Arusha
na umeme mwingine kubaki.
Ufafanuzi
huo umetolewa na mkuu wa Chuo hicho Dk
Richard Masika kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama aliyetembelea
mitambo hiyo ambayo imekabidhiwa kwa chuo hicho na Shirika la Umeme
Nchini(TANESCO)
Alisema
kuwa chuo hicho ambach kitakuwa cha kwanza barani Afrika kumiliki kituo cha
kufua umeme,kitatumia kituo hicho kwa malengo matatu ambayo ameyataja kuwa ni
pamoja na kutumika kwa mafunzo,kutengeneza vipuri vya mitambo ya umeme pamoja
na kuzalisha umeme.
Dk Masika
ameeleza kuwa baada ya kukabidhiwa kituo hicho mapema wiki iliyopita na baadaye
kuanza kazi za awali wamebaini kwamba kwa kufunga mitambo mipya ya kufua umeme
wataweza kutoa megawati 17 ambazo zitaingizwa katika gridi ya taifa.
Alisema
kuwa mitambo ya kituo hicho chenye eneo la jumla ya Ekari 400 yanategemea maji
ya mito miwili ambayo Kware unaoanzia Mlima Kilimanjaro na Mto Mbuguni unaonzia
mlima Meru ambapo maji hayo huduma katika kipindi kizima cha mwaka na
kuongezeka wakati wa kiangazi
Kwa upande
wake Mkuu wa mkoa wa Kilimanajro,Gama amewataka wataalamu wa cuo hicho pamoja
na mipango mizuri na kuonyesha kuwa na uwezo mkubwa wa kukiendesha lakini
aliwataka kuwa na uzalendo ambao utalisaidia taifa katika kutatua tatizo la
upatikanaji wa nishati ya umeme.
Kwa upande
wake Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga ameahidi kukipa ushirikiano chuo
hicho na kukitaka kuhakikisha kinaimarisha kitengo chake cha uhusiano ili kujenga
mahusiano na vijiji vinavyozunguka kituo hicho.
Makunga
alisema kuwa ni vyema chuo hicho kikajipanga kwa kushirikiana na uongozi wa
wilaya katika kuhakikisha kinawaelimisha wananchi wanaoishi maeneo ya jirani
ili watambue umuhimu wa kituo hicho na madhara ya kutaka kuingiza mifugo kwa
nguvu
No comments:
Post a Comment