Na Queen Lema,Arusha
WATENDAJI WA SACCOS WASIOKUWA NA ELIMU YA MAHESABU CHANZO
CHA SACCOS KUFA
IMEELEZWA kuwa kutokana na baadhi ya watendaji pamoja na
viongozi wa vyama vya kuweka na kukopa(SACCOS) kukosa eliumu ya mahesabu
kumesababisha sana
baadhi ya vyama hivyo kushindwa kufikia malengo yake mbalimbali ambayo yamekwa
huku pia hali hiyo ikisababisha migogoro
Hayo yameelezwa na Afisa ushirika jiji la Arusha Bw Huruma
Kibwendwa wakati akiongea na wanachama wa Saccos ya Balimi ya jijini hapa
mapema jana mara baada ya Saccos hiyo kufikia malengo yake mbalimbali
Huruma alisema kuwa kwa sasa ndani ya mkoa wa Arusha tatizo
kubwa sana ni ukosefu wa elimu ya mahesabu kwa
kuwa viongozi wengi wanaochaguliwa hawana elimu hiyo hivyo kusababisha madhara
makubwa sana
ndani ya vyama hivyo vya kuweka na kukopa
Alitaja madhara hayo kuwa ni
pamoja na migogoro ya mara kwa mara ambayo wakati mwingine husababisha
hata kufa kwa vyama hivyo, huku madhara mengine ni pamoja na kusababisha utoaji
wa mikopo ambayo haikidhi vigezo hali ambayo nayo inachangia sana hasara kubwa
sana kwenye mitaji ya vyama hivyo
“haya madhara ni makubwa sana na kwa hali hiyo basi napenda
kusema kuwa hawa viongozi wa vyama hivi wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanatafuta
elimu hii ili kuweza kunusuru vyama vya kuweka na kukopa ndani ya Jiji la
Arusha lakini kama watakuwa wanaendesha vyama vyao kwa mazoea kutasababisha
kukithiri kwa udanganyifu wa mahesabu ndani ya vyama hivyo” aliongeza Huruma
Akiongelea maendeleo ya Saccos hiyo ya Balimi Mweka hazina
wake,Bw Gerald Kazungu alisema kuwa mpaka sasa wamefanikiwa kuwa na mtaji wa
kiasi cha Milioni 73 ambapo kwa kipindi cha mwaka huu 2013 wameweza kugawa
Gawio la kiasi cha zaidi ya Milioni nane
kwa wanachama wake mara baada ya kutengeneza faida ambayo imetokana na
wanachama wake
Huruma alisema kuwa malengo halisi ya Saccos hiyo ni
kuhakikisha kuwa wanaendelea kukopesha zaidi wanachama walio wengi zaidi ambapo
kama watakuwa na wanachama wengi zaidi basi wataweza kuchangia kwa kiwango
kikubwa sana
kuokoa wananchi wa Jiji la Arusha dhidi ya Umaskini ambao unatokana na ukosefu
wa Mitaji.
Awali Mwenyekiti wa Saccos Hiyo Bw Richard Mugyabuso alisema
kuwa pamoja na kuwa wamefanikiwa kupata faida ya zaidi ya Milioni kwa kipindi
cha Miaka miwili lakini bado wakopaji walio wengi wanakabiliwa na changamoto ya
mautumizi mabaya ya mikopo hali ambayo inafanya wanakopa washindwe kurudisha
fedha hizo huku vyama navyo vikiwa vinategemea marejesho kwa ajili ya
kujiendeleza
Mugyabuso alisema kuwa wapo baadhi ya wakopaji katika baadhi
ya vyama vya kuweka na kukopa wanakopa kwa malengo kama
vile kufanya sherehe,kufikiria zaidi maisha ya kifahari,starehe huku hali hiyo
ikisababisha kushindwa kulipa hasa wanapotakiwa kulipa,huku hali hiyo
ikisababisha shuguli mbalimbali za vyama kukwama kutokana na Mtaji kupungua
badala ya kuongezeka.
MWISHO
No comments:
Post a Comment