TFDA ARUSHA YATEKEZA BIDHAA ZA MILIONI SABA
Na Queen Lema,Arusha
MAMLAKA ya Chakula na Dawa
nchini TFDA, jana imeteketeza tani moja na robo ya Shehena kubwa ya bidhaa
mbalimbali zenye thamani ya shilingi milioni 7 ambazo zimekwisha muda wake wa
matumizi na zingine hazijasajiliwa na pia hazionyeshi lini muda wake wa
matumizi utakwisha.
Akizungumza katika zoezi hilo la kuteketeza biddhaa
hizo kwenye Jalala kuu , lililopo eneo la Muriet, halmashauri ya Jiji la Arusha,
Meneja wa kanda ya Kaskazini, wa Mamlaka ya Chakula na Dawa, TFDA, ,Damas
Matiko, amesema bidhaa hizo zimekamatwa katika msako uliofanyika ndani ya wiki
moja katoka maduka ya Vyakula na Super market.jijini Arusha.
Amezitaja bidhaa hizo
zilizoteketezwa kuwa ni Mafuta ya
vyakula, Juice, Soda aina ya Pepsi zilizoko kwenye makopo, Majani ya Chai, Dawa
za miswaki za Kichina, Sukari, Maji ya Chupa, Unga wa maziwa wa uji wa watoto
uliopo kwenye makopo, Vinywaji vikali, (Pombe)
Matiko, amesema kuwa bidhaa
hizo hazikidhi viwango vuinavyotakiwa ,hazijasajiliwa na Shirika la Viwango
nchini TBS, na zingine zimeandikwa lugha isiyofahamika ,zingine zimeghushiwa
tarehe ya mwisho ya kutumika, hivyo zina madhara makubwa kwa watumiaji na pia
hazimhakikishii Usalama mlaji.
Amesema zoezi hilo la
kukamata bidhaa hizo bandia limefanyika kuanzia Februari 4 hadi February 8
mwaka huu ,ambapo Mamlaka hiyo imelazimika kuendesha msako huo kwenye maduka
baada ya kubaini kuwepo kwa bidhaa zisizokuwa na viwango na hivyo kuathiri afya
za walaji.
Matiko alitoa wito kwa wananchi
wanaonunua bidhaa zao kwenye maduka makubwa ya kuuza vyakula,{Super market},
kusoma maelezo ya bidhaa wanazonunua ili waelewe muda wa matumizi badala ya
kununua kwa haraka na kwenda kutumia wakati mwingine wanaweza kununua bidhaa
ambazo muda wake umeshakwisha na zikawa ni madhara kwao.
"wananchi wawapo na
mashaka na bidhaa hizo zilizoko kwenye maduka zikiwemo ambazo lugha na maelezo
yake hayaeleweki watoe taarifa kwa Mamlaka hiyo ya chakula na dawa TFDA, au
Idara ya afya halmashauri ya jiji la Arusha,lengo ni kulinda afyas za walaji"
alisisitiza Matiko.
Ameyataja baadhi ya madhara
hayo kuwa ni pamoja na kupata magonjwa kama vile Saratan, kuharisha ,maumivu ya
tumbo ,kupata mzio unaotokana na kula vyakula vya aina Fulani, wengine hunenepa
na kuwa na miili mikubwa mfano kwa wanawake.
Kwa upande wake kaimu afisa
afya mkuu wa jiji la Arusha, Alan Sumari, mewataka wafanyabiashara kuingiza
nchini bidhaa zenye viwango ili kuepuka hasara ya bidhaa hizo kuteketezwa na Mamlaka
ya Chakula na Dawa TFDA.
No comments:
Post a Comment