TANZANIA
YAINGIA KWENYE MAAJABU SABA YA AFRIKA
Na Queen Lema,Arusha
TANZANIA
kupitia shirika la Hifadhi za Taifa limefanikiwa kuingia katika maajabu saba
katika bara la Afrika hali ambayo itafanya Sekta ya utalii hapa nchini iweze
kukua na kuimarika sana
tofauti na hapo awali.
Akitangaza Vivutio hivyo vitatiu mjini hapa mapema jana Dr Philiph
Imler ambaye ni mwanzilishi na raisi wa maajabu saba barani Afrika alisema kuwa
Tanzania
kwa wakati huu umefanikiwa kupata vivutio vitatu
Alitaja vivutio hivyo kuwa ni Pamoja na Mlima
Kilimanjaro,hifadhi ya Serengeti pamoja na bonde la Ngorongoro ambapo vivutio
hivyo viliweza kupigiwa kura nyingi sana na hivyo kuvipa ushindi wa hali ya juu
kwa pia ndani ya vivutio hivyo kuna maajabu ya aina mbalimbali ambayo
hayapatikani popote barani Afrika na duniani kwa ujumla
“leo nina furai kutangaza kuwa Tanzania imeingia ndani ya
maajabu saba na hivyo basi hii ni kama changamoto ya kuhakikisha kuwa bado
mnaendelea kufanya viendelee kukua na kuinarika zaidi ili hata wakati mwingine
muwe na vivutio vingi zaidi’aliongeza Dkt Imler.
Katika hatua Nyingine Waziri mkuu wa Tanzania,Mizengo Kayanza Pinda alisema kuwa bado
Nchi za Afrika zinahitaji zaidi kuwekeza zaidi katika masuala ya Utalii ikiwa
ni pamoja na kuongeza zaidi jitiada za utalii kwani bado kuna changamoto kubwa sana katika masuala ya
utalii.
Pinda aliongeza kuwa endapo kama Nchi hizo zitaweza kufanya
hivyo basi Nchi hizo zitakuwa na Vivutio venye maajabu mengi sana
duniani hali ambayo nayo itachangia sana
kuweza kuimarisha utalii wa ndani na hata wa nje ya nchi husika.
Aliongeza kuwa ndani ya Nchi
ya Tanzania kwa sasa
wamejiwekea juhudi za makusudi kuanzia ngazi ya kitaifa ambapo kupitia ngazi
mbalimbali wataweza kuharakisha maendeleo ya utalii hususani utalii ili maajabu
mbalimbali ya Tanzania
yaweze kufahamika duniani.
Awali mkurugenzi wa shirika la hifadhi za Taifa hapa
nchini(TANAPA)Alan Kijazi alisema kuwa wanatarajia mapato kuongezeka hasa katika
mlima Kilimanjaro,bonde la Ngorongoro,
na hifadhi za Serengeti kwa kuwa vivutio hivyo vimetangazwa rasmi kama vivutio
venye maajabu ya kutosha
Kijazi alisema kuwa pamoja na kutangazwa kwa vivutio hivyo
lakini bado TANAPA limejiwekea mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa
wanaendeleza shuguli za utalii hapa nchini ingawaje bado kuna changamoto kubwa sana kwenye masuala ya
utalii wa ndani
MWISHO
No comments:
Post a Comment