Monday, December 19, 2011

TRA ARUSHA YAFANIKIWA KUWAFARIJI WATOTO YATIMA




Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoani Arusha imetoa misaada yenye thamani ya zaidi  sh.miloni moja na nusu kwa vituo vya watoto yatima  ikiwa ni kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya mlipa kodi.

Akikabidhi misaada hiyo meneja mkoa wa Arusha Evaristo Kileva alisema kuwa misaada hiyo ni njia mojawapo ya kuhakikisha kuwa mamlaka inatoa msaada kidogo ili kuwapa nguvu wanajamii wenye mioyo ya kufanya kazi.

Kileva alisema kuwa mamlaka inatambua mchango wa walipa kodi hivyo iliona ni muhimu wiki  ya maadhimisho ya mlipa kodi iwatembelee watoto  yatima kwa kuwapatia misaada mbalimbali ili iweze kuwasaidia na kutambua kuwa mamlaka ipo pamoja nao.

Aidha ameongeza kuwa watoto yatima ni taifa la kesho hivyo wakilelewa katika mazingira mazuri ikiwa ni pamoja na kupata chakula,elimu bora, malazi na mavazi  basi ni wazi wataongeza juhudi katika masomo yao hali itakayowezesha taifa la kesho kuwa lenye jamii iliyoelimika.

Hata hivyo amewataka watanzania,mashirika na taasisi mbalimbali kuwaunga mkono vituo vya watoto yatima kwa kuchangia hata kidogo walichonacho kwani watoto hao wanahaki sawa ya kupata elimu bora kama watoto wengine.

Naye mkurugenzi wa kituo cha Nora Children Care Trust ambacho ni miongoni mwa kituo kilichopatiwa msaada bi.Nora Anthon alisema kuwa changamoto kubwa ni pamoja na ukosefu wa  kuwapatia watoto elimu,chakula,matibabu na usafiri  kutokana na kituo kukosa mradi.

Hata hivyo misaada  iliotolewa ni pamoja na mchele,maharagwe,unga wa lishe,unga wa sembe,maziwa,sukari,madaftari,mashuka,mablanketi,sweta za shule,mafuta ya kupikia,sabuni,na kalamu.

Vituo vilivyopatiwa misaada ni pamoja na nora children care kilichopo eneo la makumira nje kidogo ya jiji la Arusha na kituo cha yatima cha The Christian women emancipation organization kilichopo sinoni ungalimited.

Mwisho……

CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA

0758907891

ARUSHA

No comments:

Post a Comment