Tuesday, April 9, 2013

TUMIENI KAMUSI HATA MNAPOKUWA MADHABAHUNI-JOKA KUU


TUMIENI KAMUSI HATA MNAPOKUWA MADHABAHUNI-JOKA KUU

Na Bety Alex,Arusha

Mchungaji Herbert Anthony”Joka kuu”amewataka watumishi wa Mungu kuhakikisha kuwa wanafundisha masomo yao ya kila siku kwa waumini wakiwa na uhakika wa maneno lakini kama hawana uhakika basi wahakikishe kuwa wanatumia kamusi ili kujiepusha na tabia ya kupotosha maana ambazo wakati mwingine zinachangia sana kumtukuza Shetani kwa siri.

Kwa sasa hata unaposema neno unatakiwa kujua maana ya lile neno ambalo umelisema kwa kuwa maneno ya sasa yanachukuliwa kivingine kabisa  lakini kama mtumishi wa  Mungu unashindwa kujua na kutambua  maana basi tumia hata kamusi

Joka kuu aliyasema hayo jijini hapa wakati akiongea na waumini wa kanisa hilo mapema wiki hii  katika somo lilolokuwa lina husuurejesho wa afya ambapo alidai kuwa hata maneno ya sasa yanatakiwa kuchunguzwa kabla ya kutamkwa

Alidai kuwa kwa kutumia kamusi kutaweza kuwafundisha wakristo  maneno ambayo yana maana lakini kama watumishi wa mungu watakuwa wanachukua maneno bila ya kuyachuja kutasababisha mafundisho ambayo wanayatoa kwenye ibada zao  ya bure huku watu wakizidi kuangamia zaidi katika dhambi

“dunia ya sasa kwa kweli imebadilika sana hivyo basi kuliko uhubiri neno ambalo hujui maana yake ni bora unyamaze kimya kabisa unakuta mtumishi anasema kuwa ninyi ni wajanja akijua kuwa mjanja ni mtu mwenye kiwango bora kumbe neno mjanja linamaanisha mtu tapeli tapeli,sasa hapa unaona kuwa shetani anaweeza kutawala badala  Mungu aweze kutawala”aliongeza Joka kuu

Awali akiongelea  somo hilo la Urejesho wa afya ndani ya jamii ya sasa alidai kuwa Tanzania ya leo imekumbwa na magonjwa mengi sana kwa kuwa wengi wamesahau kweli ya Mungu tofauti na Miaka iliyiopita ambapo magonjwa hayo wakati mwingine chanzo chake kikubwa ni Dhambi

Alifafafnua kuwa dhambi zinapozidi maali basi kinachofuata hapa ni magonjwa  na mateso ya kila siku lakini kwa sasa wakristo pamoja na watanzania kwa ujumla wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanarejea katika torati ya bwana ili bwana mwenyewe aweze kupunguza kasi ya magonjwa ambayo ndio umaskani wa baadhi ya watu.

“ukiangalia kwenye vyombo vya habari ubakutana na mambo na unyama wa hali ya juu sana ambao unafanywa na watu ambao mwisho wake huishia kusababisha kilema cha ugonjwa sasa  inabidi wakristo tuamke na tukatae hali kama hizi na badala yake turudi katika torati’aliongeza Joka kuu

Alimalizia  kwa kuwataka wakrsito wahakikishe kuwa wanafanya urejesho na kuachana na tabia ya kuchukulia  lugha na mambo mengine kiraisi bali wahakikishe kuwa wana ishi vema ikiwa ni pamoja na kutojihusishaa na dhambi ambazo ambazo ndizo zinazozaa maovu katika dunia

MWISHO

ASKOFU SIXBERT ATANGAZA KURUDISHA AMANI YA ARUSHA


ASKOFU SIXBERT ATANGAZA KURUDISHA AMANI YA ARUSHA

Na Bety Alex,Arusha

KANISA  la Victorius Church  Hema ya Ukombozi  Sakina limetangaza kuwa kwa sasa ndani ya Mji wa Arusha hakutakuwa na maasi mbalimbali ikiwa ni  pamoja na vita ambavyo vinasababishwa na mambo mbalimbali na badala yake  historia mbaya ya mji wa Arusha itafutika na historia ya amani itaaanza kujiandika yenyewe

Akiongea na “nyakati”mara baada ya kuwekwa wakfu na kuzinduliwa kwa kanisa  na hema hilo jipya lililopo maeneo ya Sakina askofu wa kanisa hilo Sixbert Paul alisema kuwa ameingia rasmi ndani ya mji wa Arusha hivyo  ni lazima mabadiliko yaanze kuonekana

Askofu huyo alidai kuwa amepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge hivyo ni lazima mji uweze kurudisha heshima yake ambayo ulikuwa umepewa ikiwa ni  pamoja na kupunguza na kuondoa idadi ya maovu ambayo yanatokea zaidi katika mji wa Arusha

Alifafanua kuwa kupitia madhabahu yake ni lazima uponyaji tena wa hali ya juu sana uweze kutembea na pia uweze kuokoa watu ili lengo lake halisi liweze kufikiwa na faida za madhabahu yake ziweze kiutumika hata na viongozi wa kila aina huku hali hiyo pia ikichangia uwezo wa kumrudishia Mungu sifa na utukufu

“nimekuja Arusha rasmi sasa ni lazima kila roho ambayo iko kinyume na mapenzi ya Mungu iweze kusalimu amri na kuondoka nataka historia mpya kwenye maisha ya kila mtanzania wa Arusha.kwa hiyo watu waanze kujiandaa kwa  uponyaji na amani ya mkoa wa huu”aliongeza Askofu huyo

Pia alisema kuwa kupitia madhabahu yake ni Lazima hata hali ya maisha ya wakazi wa mji wa Arusha iweze kubadilika tena kwa kiwango cha hali ya juu sana na kila mtanzania kuwa na maisha yenye ubora na uhakika wa kiwango cha hali ya juu kwa kuwa madhabahu yake inatenda.

“kazi kubwa ya madhabahu hii ni kufungua watu katika shida na kisha kuwaweka huru hivyo kama watawekwa huru ni raisi sana kwao kuhakikisha kuwa wanakula mema ya nchi yaani maisha yao yawe na ubora wa hali ya juu na kuachana na maisha ya shida ambayo yana mwanzo na pia yana mwisho”alisema

Hataivyo wakristo mbalimbali ambao walihudhuria uzinduzi huo walisema kuwa wanaratarajia kuona mabadiliko makubwa sana ambayo yatasababishwa na hema hilo kwa kuwa hapo awali Arusha ilikuwa na Vita kubwa sana ya kisiasa hali ambayo ilipoteza maana halisi ya Arusha na hivyo kusababisha umaskini mkubwa kwa baadhi ya watu wakiwemo wafanyabiashara.

MWISHO

INSERT KWA KUSHIRIKIANA NA JUKWAA LA WAZEE LATARAJIA KUJENGA KITUO CHA WAZEE WA MKOA WA ARUSHA


INSERT KWA KUSHIRIKIANA NA JUKWAA LA WAZEE LATARAJIA KUJENGA KITUO CHA WAZEE  WA MKOA WA ARUSHA

Asasi ya Informal Sector team(INSERT)Kikiana na jukwaa la  wazee wa mkoa wa Arusha wanatarajia kujenga kituo kwa ajili ya makazi ya wazee ambapo kituo hicho kitagarimu kiasi cha zaidi ya Milioni 150 huku lengo likiwa ni kusaidia wazee ambao hawana uwezo ndani ya mkoa wa Arusha

Akizungumza katika jukwaa la wazee wa mji wa Arusha (JUWA) mratibu wa  jukwaa hilo bw  Javes Sauni alisema kuwa mpaka sasa kuna mikakati mbalimbali ya kuanza marra moja ujenzi wa kituo hicho cha wazee kwa mkoa wa Arusha

Alitaja kuwa mikakayi hiyo inasema kuwa kituo hicho cha wazee kitajengwa katika eneo la Kisongo ambapo kituo hicho kwa mara ya kwanza kitaweza kuhudumia wazee zaidi ya 60  hasa wale ambao wanatoka katika mazingira magumu

Aliongeza kuwa endapo kama mpango huo wa hivi karibuni utaweza kufikiwa tena kwa haraka basi utaweza kuwa  na faida kubwa sana kwa wazee wa mkoa wa Arusha kwa kuwa baadhi yao wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha huku wengine  nao wakiwa wanakabiliwa na ukosefu wa mahala pa kuishi

“hili jukwaa la wazee limeona kuwa upo umuhimu tena mkubwa sana wa kuhakikisha kuwa tunaangalia zaidi maslahi ya wazee hasa wale ambao wanatokea katika mazingira magumu lakini njia mojawapo ya kuweza kuwasaidia wazee hawa ni kuhakikisha kuwa kwa kiasi Fulani wanakuwa na kituo ambacho kama sio kukutanika pale na kuongea masuala yao ya wazee lakini pia kitasadiia sana kuokoa maisha ya wengi”aliongeza Sauni

Wakati huo huo alisema kuwa kwa sasa bado asilimia kubwa sana ya wazee hasa wa mji wa Arusha wanakabiliwa na changamoto kubwa sana ya matibabu hali ambayo wakati mwingine husababisha vilema vya kudumu au vifo hasa kwa wazee ambao wanatoka katika familia ambazo hazina uwezo

Pia alisema kuwa kutokana na changamoto hiyo watatumia jukwaaa la wazee kwa kuhakikisha kuwa wanatafuta mbinu mbadala ambazo zitaweza kuwaokoa wazee hasa wale ambao hawana uwezo wa kujitibu ikiwa ni pamoja na kukosa hata fedha kwa ajili ya manunuzi ya dawa

“hii ni changamoto kubwa sana ambayo inawakabili wazee wa mkoa wa Arusha lakini tutatafuta mbinu mbadala na kuhakikisha kuwa wazee wanapata matibabu kwa kuwa tayari Serikali ilishatoa Agizo lakini vituo vya afya vya  Mjini hapa bado havitekelezi sera hiyo pamoja na Tamko hilo”alifafanua  Bw Sauni

ASKOFU ALITAKA TAIFA LA TANZANIA KUTOJIBU VITA YA MASHAMBULIZI YA AINA YOYOTE ILE


ASKOFU ALITAKA TAIFA LA TANZANIA KUTOJIBU VITA YA MASHAMBULIZI YA AINA YOYOTE ILE

TAIFA la Tanzania pamoja na watu wake wameaswa kuachana  na tabia ya kulipizana kisasi cha aina yoyote ile badala yake lihakikishe kuwa linalipa ubaya kwa wema hali ambayo itaweza  kuwanyanya watanzania dhidi ya machafuko mbalimbali yanayoendelea ndani na nje.

Kauli hiyo imetolewa Mjini Arusha mapema jana na  askofu wa kanisa Katoliki Jimbo la Arusha,baba askofu Josephat Lobulu wakati akiongea na vyombo mbalimbali vya habari kuhusiana na maazimisho ya miaka 50 ya kanisa hilo yanayoendelea mjini hapa

Askofu huyo alisema kuwa kwa sasa Nchi ya Tanzania imekumbwa na machafuko mengi sana lakini si jambo jema kama wananchi au taifa litaachia amani  na kisha kuingia kwenye malumbano ambayo wakati mwingine yanasababisha maafa hata kwa wasio kuwa na hatia

Alifafanua kuwa kamwe jambo baya haliwezi kuisha kwenye jamii kama litalipzwa kwa ubaya bali jambo baya litaweza kuisha endapo kama litalipzwa zaidi kwa wema huku wema huo ukiwa ni viashiria vya amani ambayo wakati mwingine inapotea kutokana na ubaya ambao umo kwenye jamii

“kama nchi ya Tanzania tutataka kupoteza amani basi tuanze kuyafuta na kutafuta vyanzo vya vitu mbalimbali ambavyo vimezaa maovu ni wazi kuwa damu za watu wasiokuwa na hatia zitamwagika bure sasa mimi nawasihi sana watanzania wahakikishe kuwa wanalinda amani yao na wasiwe chanzo cha kuharibu amani ya taifa lao”aliongeza Askofu Lobulu

Akiongelea Sekta  za elimu na afya ambazo zimo chini ya kanisa hilo alisema kuwa mpaka sasa kanisa hilo hususani kwa mkoa wa Arusha limeshaweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa wanatoa elimu kwa watanzania ambapo elimu hiyo pia itaweeza kupambana na adui Ujinga pamoja na adui Umaskini

Aliongeza kuwa kwa kuwa na sekta nzuri ya elimu ambayo itaweza kuwaruhusu watanzania kujipatia elimu pia kutaweza kuraisisha maisha ya vijana wa kitanzania ambapo kama watakuwa na elimu ya kutosha basi wataweza kukimbia hata maasi ya Taifa ambayo wakati mwingine yanatokea kwa kuwa hakuna kazi za kufanya


“tumedhamiria kuwa kwa sasa tunataka tuwe na elimu ya juu lakini pia hata kuweza kuiboresha zaidi ambapo itatoa fursa kwa vijana wengi zaidi lakini pia tutaweza kufikia malengo yetu ambayo tumejiwekea ya kutaka kuwafanya vijana wa kitanzania kuwa na elimu kama zilivyo nchi nyingine “alibainisha Askofu Lobulu

MWISHO

Friday, April 5, 2013

KAMPUNI YA CHICO YATOA RAMBIRAMBI


MH WAZIRI MKUU APOKEA SHILINGI MILIONI KUMI ZA RAMBIRAMBI KUTOKA KAMPUNI YA CHICO KUTOKANA NA AJALI YA KUANGUKA KWA JENGO JIJINI DAR ES SALAAM


ARUSHA INAKABILIWA NA ONGEZEKO KUBWA LA UHITAJI WA MAJI




ARUSHA INAKABILIWA NA ONGEZEKO KUBWA LA UHITAJI WA MAJI

NA BETY ALEX
,Arusha


Jiji la Arusha linakabiliwa na changamoto ya ongezeko kubwa la uhitaji wa maji kutoka mita za ujazo 53,030  hadi mita za ujazo 93,270 kwa siku  kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watu inayokua kwa kasi isiyoendana na kiwango cha uzalishaji wa maji.

Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya maji safi na maji taka Arusha (AUWSA) mhandishi Ruth Koya katika Kilelecha Wiki ya maji iliyoadhimishwa Jijini hapa Mwishoni mwa wiki

Alisema  kuwa Kiwango cha uzalishaji wa maji  kimeshuka kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi yaliyosababisha ukame  na kiwango hicho kushuka hadi kufikia mita za ujazo 32,000 hadi 45,000 kwa siku,hali hiyo inailazimu mamlaka husika kuwa na mgao wa maji hasa katika maeneo yaliyoinuka na yale yaliyoko pembezoni mwa jiji  kama Mbauda,Ngusero,Sombetini,Morombo na Terrat.


Mhandisi Koya aliendelea kwa kusema kuwa hali hiyo inasababishwa na ukuaji wa mji wa Arusha kutokana na kuongezeka  kwa shughuli za kijamii na za kiserikali.Hivyo kwa ujumla mamlaka yake inakabiliwa na changamoto ya kuendelea kutafuta vyanzo vipya vya maji ili kukidhi ongezeko  kubwa la mahitaji ya maji.

Mbali na hayo alisema kuwa  mamlaka hiyo imekuwa na mikakati ya muda mrefu na muda mfupi ya kukabiliana na ongezeko la uhitaji wa maji kama vile uendelezaji wa chem chem za Machare zilizoko kata ya Moshono ambazo mamlaka inaendelea kuiboresha inatoa lita 30,000 kwa saa, pamoja na kuchimba visima vipya katika kata ya Sokon 1,Engutoto na Sombetini.

Akizungumzia changamoto zinazoikabili mamlaka hiyo,Mkurugenzi huyo amesema kuwa  wananchi wamekuwa wakivamia  maeneo ya vyanzo vya maji kwa ajili ya shughuli za kibinadamu  kama vile kilimo,ufugaji,uvunaji miti,uharibifu wa mazingira kwa ujumla.


Naye  Mwenyekiti wa bodi  wa mamlaka hiyo bwa  Felix Mrema alisema kuwa vyanzo vya maji vinazidi kupungua kila siku na mahitaji ya maji yanazidi kuongezeka na kueleza kuwa suluhu ya tatizo hili ni serikali kufanya jitihada za makusudi  za kuyahifadhi maeneo ya vyanzo yasiingiliane na shughuli za binadamu akitolea mfano eneo la Burka na Ngaramtoni ambalo amedai kuwa  linaweza kutosheleza mahitaji ya maji kwa jiji la Arusha kwa miaka 50 ijayo.


 Aliwataka wananchi wa Mkoa wa Arusha kuhakikisha kuwa wanajiwekea utaratibu wa kueshimu zaidi vyanzo vya maji na kuachana na tabia ya kuharibu vyanzo hivyo kwani uharibifu huo mara nyingine ndio chanzo kikubwa cha ukame ndani ya Jiji la Arusha

CHUO CHA UFUNDI ARUSHA CHAANZA MKAKATI WA KUFUA MITAMBO YA UMEME

CHUO CHA UFUNDI ARUSHA CHAANZA MKAKATI WA KUFUA MITAMBO YA UMEME






Chuo cha Ufundi Arusha kimeanza mkakati wa kufufua mitambo ya kuzalishia umeme wa maji wa Kituo cha Kikuletwa iliyopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro ambapo hadi itakapokamilika itaweza kutosheleza mahitaji ya mikoa ya Kilimanjaro na Arusha na umeme mwingine kubaki.

Ufafanuzi huo umetolewa na  mkuu wa Chuo hicho Dk Richard Masika kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama aliyetembelea mitambo hiyo ambayo imekabidhiwa kwa chuo hicho na Shirika la Umeme Nchini(TANESCO)

Alisema kuwa chuo hicho ambach kitakuwa cha kwanza barani Afrika kumiliki kituo cha kufua umeme,kitatumia kituo hicho kwa malengo matatu ambayo ameyataja kuwa ni pamoja na kutumika kwa mafunzo,kutengeneza vipuri vya mitambo ya umeme pamoja na kuzalisha umeme.

Dk Masika ameeleza kuwa baada ya kukabidhiwa kituo hicho mapema wiki iliyopita na baadaye kuanza kazi za awali wamebaini kwamba kwa kufunga mitambo mipya ya kufua umeme wataweza kutoa megawati 17 ambazo zitaingizwa katika gridi ya taifa.



Alisema kuwa mitambo ya kituo hicho chenye eneo la jumla ya Ekari 400 yanategemea maji ya mito miwili ambayo Kware unaoanzia Mlima Kilimanjaro na Mto Mbuguni unaonzia mlima Meru ambapo maji hayo huduma katika kipindi kizima cha mwaka na kuongezeka wakati wa kiangazi

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Kilimanajro,Gama amewataka wataalamu wa cuo hicho pamoja na mipango mizuri na kuonyesha kuwa na uwezo mkubwa wa kukiendesha lakini aliwataka kuwa na uzalendo ambao utalisaidia taifa katika kutatua tatizo la upatikanaji wa nishati ya umeme.


Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga ameahidi kukipa ushirikiano chuo hicho na kukitaka kuhakikisha kinaimarisha kitengo chake cha uhusiano ili kujenga mahusiano na vijiji vinavyozunguka kituo hicho.


Makunga alisema kuwa ni vyema chuo hicho kikajipanga kwa kushirikiana na uongozi wa wilaya katika kuhakikisha kinawaelimisha wananchi wanaoishi maeneo ya jirani ili watambue umuhimu wa kituo hicho na madhara ya kutaka kuingiza mifugo kwa nguvu

ANDIKENI HABARI ZA UCHUNGUZI ZAIDI ACHANENI NA HABARI ZA SEMINA NA MIKUTANO- MWOLEKA


ANDIKENI HABARI ZA UCHUNGUZI ZAIDI ACHANENI NA HABARI ZA SEMINA NA MIKUTANO- MWOLEKA



Kushoto ni Malkia  wa  Matukio Arusha, na kulia ni Rose Jackson wakiwa wanatafakari jambo katika mtandao,hawa pia ni baadhi ya waandishi wa habari pia wakiwa kazini


Na Gladness Mushi,Arusha

WAANDISHI wa habari hapa Nchini wameaswa kuhakikisha kuwa wanajiwekea utatibu wa kuandika zaidi habari za uchunguzi kuliko kurtegemea habari za semina na mikutano kwani habari za mikutano na semina bado hazitoi majawabu na changamoto kwa jamii

Endapo kama waandishi wa habari wa Tanzania wataweza kujiwekea utaribu wa kuandika habari ambazo zina uchunguzi wa kutosha basi watakuwa ni chanzo kikubwa sana cha maendeleo ya Nchi

Hayo yalielezwa Jana na Anjelo Mwoleka ambaye ni Mkurugenzi wa Jambo  Arusha Publisher wakati  akiongea na wahitimu wa fani ya uandishi wa habari katika chuo cha uandishi wa habari Arusha (AJTC) katika maafali ya sita ya chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo.

Aidha Mwoleka alisema kuwa kwa sasa kuna wimbi kubwa la waandishi wa habari a wanajihusisha zaidi na masuala ya habari za Semina na kuachana na habari za kiuchunguzi hali ambayo wakati mwingine ina nyima haki za msingi za jamii kwa kuwa waandishi wa habari wana nafasi kubwa sana ya kuibua maovu yanaoendelea kwenye Jamii

Alifafanua kuwa habari za uchunguzi ndani ya Nchi ya Tanzania ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi hivyo basi wana habari hawapswi kukimbia na badala yake wanapswa kuzipa kipaumbele kikubwa ili kuweza kuruhusu changamoto kwenye sekta zote kujilikana

“kuwa mwandishi wa habari sio lazima uwe unajua ratiba za mikutano za kila siku bali kuna maana kuwa unapaswa kujua na kutambua kuwa unatakiwa lkuwa mchunguzi na hapo ndio kazi yako itakuwa na manufaa makubwa sana kwa jamii hivyo basi habari za muhimu zinatakiwa kupewa kipaumbele tena kikubwa sana ili nchi ya Tanzania iweze kufika mahali ambapo inatakiwa kufika kama zilivyo nchi nyingine ambazo zimeendelea duniani”aliongeza Mwoleka


Awali wahitimu wa mafunzo hayo ya uandishi wa habari katika ngazi ya cheti, na shahada walisema kuwa pamoja na kuwa chuo hicho kimewalea katika maadili mazuri lakini bado wanakabiliwa na uhaba wa vifaa kama vile Kompyuta, na Kamera kwa ajili ya mazoezi.