WANANCHI wenye hasira katika eneo la Ngusero Ndani ya
manispaa ya Arusha wamewaua majambazi matatu kwa silaha za jadi mara baada ya
majambazi hayo kubainika kuwa wanapanga mbinu mbalimbali za kuvunja nyumba
Akiongea na waandishi wa habari mapema leo kamanda wa polisi
wa mkoa wa Arusha Bw Thobias Andengenye alisema kuwa tukio hilo
lilitokea alfajiri ya saa kumi za asubui ambapo majambazi hayo yalifika katika
eneo hilo huku
yakiwa ndani ya gari
Kamanda Andengenye alisema kuwa mara baaada ya majambazi
hayo kufika katika eneo hilo la tukio wakiwa na
gari aina ya Corola lenye namba T830 AHU walianza kuzunguka zunguka katika eneo
hilo ili
kupanga nyumba ambayo wanaingia hali ambayo iliwashitua wananchi
Alifafanua kuwa mara baada ya wananchi kutilia shaka gari
hilo ambalo lilikuwa na majambazi hao waliamua kuwaweka chini ya ulinzi na
kukagua gari hilo ambapo walikutana na Silaha za jadi pamoja na silaha nyingine ambazo ni za
kuvunjia nyumba hali ambayo ilisababisha
waweze kupigwa sana na wananchi hao
“inavyosemekana ni kwamba hawa majambazi walikuwa
wameshazunguka san a na gari lao kwa muda mrefu sana na sasa mara baada ya
kuhisiwa wananachi waliamua kujichukulia sheria mkononi na kisha kuanza
kuwapiga sana hali ambayo ilisababisha Mauti yao hapo hapo”alisema kamanda
Andengenye.
Aliongeza kuwa mara baada ya Jeshi la Polisi kufika katika
eneo hilo waliweza kugundua kuwa kati ya
majambazi hayo matatu mawili yalikuwa yanatafutwa na jeshi hilo bila mafanikio kwa kuwa walikuwa
wanatuhumiwa kwa makosa ya unyanganyi wa kutumia silaha ndani ya maeneo
mbalimbali ya Mji wa Arusha
Pia alisema kuwa majambazi hayo yalifajhamika kwa majina ya Philipho Naftari,huku jambazi
mmoja amejulikana kwa jina la Utani ambalo ni shidaa na mwingine hajajulikana
jina lake huku jitiada za kuwatafuta ndugu zake
zikiwa zinaendelea.
Hataivyo kamanda huyo alisema kuwa pamoja na kuwa waliowawa
walikuwa ni majambazi lakiniPolisi inatafuta chanzo halisi cha aliyeanzisha
kipigo na kusababisha wengine kuwauwa majambazi hayo kwa kuwa wengeweza
kusaidiasana polisi katika upelelezi wao
lakini kwa kuwa wameshawauwa hakuna upelelezi
tena
Wakati huo huo Jeshi la Polisi mkoani Arusha linamshikilia
mkazi mmoja wa longido kwa kosa la kumsukuma Rafiki yake na kisha kudondoka na kupoteza maisha papo hapo katika
baa moja iliyojulikana kwa jina laZebra.
Kamanda Andengenye alisema kuwa tukio hilo lilitokea May 20 majira ya saa kumi za jioni ambapo mtu
mmoja liyefhamika kwa jina la Abuu Msema alifariki dunia mara baada ya
kusukumwa na rafiki yake ambaye aliyejulikana kwa majina ya Frank Mmasi mkazi wa Longido mjini hapa
Alisema kuwa katika siku hiyo ya tukio Marehemu akiwa na rafiki yake wakiwa ndani
jya baa ya Zebra walikunywa pombe sana linaendelea
na upelelezi zaidi kuhusiana na tukio hilo
huku mtuhumiwa naye akiendelea kuhojiwa juu ya mauaji hayo na atafikishwa
mahakamani upeleezi utakapokamilika.
lakini marehemu alikataa kuondoka huku rafiki yake akimtraka
aondoke hali ambayo ilimfanya amnyanyue kwa nguvu huku akiwa amelewa na badaye
alidondoka chini na kufariki dunia papo hapo