Raisi Jakaya Kikwete
KANISA la T A G Patmo
nkoanekoli lilopo Wilayani meru mkoani arusha limeweka mikakat
mbalimbali ya kuombea uchaguzi wa taifa la Tanzania ambao unatarajiwa
kufanyika mapema mwakani 2015
Aidha uamuzi huo wa kufanya maombi ambayo yanafanyika kila
mwanzo wa mwezi ili kuweza kuraishsisha uchaguzi huo wa wabunge pamoja
na madiwani wa kata zote
Akiongea kanisani hapo kwenye
ibada ya siku ya jumapili ambayo iliongozwa na neno la mungu la
kuwahimiza wakristo kutojiinua mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Japheti
Nanyaro alisema kuwa utararibu huo utaweza kuwasaidia sana taifa
nanyaro alisema kuwa,maombi hayo ambayo yanafanywa na kanisa
hilo yanalenga sehemu mbalimbali ambazo ni muhimu sana kwenye maisha ya
kiroho ya mkristo wa sasa
alitaja kuwa wakati wa
uchaguzi na kampeni mbalimbali za nchi panakuwa na roho lukuki za
kishetani ambazo zinaibuka ambapo pia wakati mwingine roho hizo
husababisha hata baadhi ya damu ambazo hazina hatia kuweza kuibuka na
kufanya kazi
aliongeza kuwa mbali na roho hizo kuweza kuibuka lakini pia
wakati mwingine kuna kuwa na maroho ya kuwanyima haki wanyonge hasa wale
ambao wameitwa na Mungu kutokana na watu ambao wapo kuweza kutumia veo
vyao kuiba haki
pia aliongeza kuwa nayo makanisa mengine yanatakiwa
kuhakikisha kuwa yanaweka utaratibu wa kuweza kuomba juu ya matukio ya
kitafia ndanui ya nchi kwani wakati mwingine roho za kujiinua nazo
zinachangia sana hata wananchi kukosa haki zao za msingi
mbali na hayo pia aliwataka nao wakristo kuhakikisha kuwa
wananchana na tabia ya kujiinua kutokana na vyeo vyao vya kanisa lakini
hata vile vya kidunia kwani hali hiyo imesababisha walio wengi sana hasa
wale wenye tabia hizo kuangamia bila kujijua
"nawasihi sana hakikisheni kuwa kamwe hamujiinui bali
mnainuliwa na bwana mwenyewe ili msiweze kushuka ila mkjiinua na kutumia
njia za mkato kwenye maisha au uongozi wa maisha yenu ya kila siku ni
lazima mtapata shida na mtadhalilika sana subirini neema ya bwana iweze
kukufika kwenye kila jambo"aliongeza Nanyaro
MWISHO
No comments:
Post a Comment