IMEELEZWA
kuwa asilimia kubwa ya watanzania wamekuwa
hawapati nafasi mbalimbali za ajira kwenye mahoteli kutokana na wengi
wao kutokuwa na elimu ya kutosha na
hivyo kuchangia wageni kutoka nje ya nchi kupata ajira kwa urahisi .
Aidha hali
hiyo imekuwa ikichangia kwa kiasi kikubwa sana vijana wengi kukosa ajira katika
mahoteli kutokana na wengi wao kutokuwa na elimu ya vitendo na hivyo kuishia kutumia elimu ya
darasani.
Hayo
yalisemwa jana na Meneja wa
programu wa shirikisho la vyama vya
utalii Tanzania (TCT) Fatma Mabrouk alipokuwa akizungumza na wamiliki wa mahoteli
jijini Arusha wakati wa kuutambulisha programu ya mafunzo kazini ambayo itawanufaisha vijana wenye umri
wa miaka 17-25.
Alisema
kuwa, programu hiyo kwa sasa ipo katika hatua ya majaribio kwa miaka miwili ambapo wameanzia jijini Dar
es Saalamu kwa kuzungumza na wamiliki wa
mahoteli kwa lengo la kuitambulisha programu hiyo ili waweze kuitumia kwa
wafanyakazi wao na kuongeza ufanisi na
utendaji kazi zaidi.
Fatma
aliongeza kuwa,programu hiyo itasaidia kuwaongezea wafanyakazi wa mahoteli
ujuzi zaidi katika utendaji kazi wao kwani wengi wao hawana ujuzi huo hali inayochangia wengi wao kushindwa
kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
‘kwa sasa
hivi wengi wao wanajifunza masomo ya darasani kwa asilimia 70 huku makazini
wakitumia asilimia 30 tu, hali ambayo inaadhiri utendaji kazi wao kwa kiasi
kikubwa kutokana na kutumia muda mwingi darasani badala ya makazini’alisema Fatma.
Naye
Mkurugenzi mtendaji wa chama cha mahoteli
Tanzania(HAT) ,alisema kuwa,Lathifa Sykes alisema kuwa,baada ya muda
majaribio kumalizika programu hiyo itapitishwa kuwa sheria na hatimaye kuweza
kutumika katika vyuo mbalimbali vya utalii hapa nchini .
Sykes
aliongeza kuwa,kwa sasa vyuo vingi vya utalii vimekuwa vikitoa elimu hiyo kwa
njia tofauti tofauti na hivyo kupitia programu hii itasaidia kufundisha kitu
kimoja kwa vyuo vyote na hivyo kuwawezesha wanafunzi hao kupata ujuzi
unaohitajika katika soko la hoteli.
Alisema
kuwa,programu hiyo inafadhiliwa na shirika la kazi duniani (ILO) ambapo lengo
halisi ni kuhakikisha kuwa idadi ya wafanyakazi kwenye mahoteli inaongezeka .
Mwisho.
No comments:
Post a Comment