Wednesday, March 5, 2014

CCM WAWAFARIJI WAGONJWA

MWENYEKITI WA CCM TAIFA, JAKAYA KIKWETE

CHAMA  cha Mapinduzi Wilaya ya Karatu mkoa wa Arusha kimefanikiwa kutoa msaada kwa wagonjwa zaidi ya 100  wa hospitali teule ya wilaya ya Karatu(DDH KARATU)huku lengo likiwa ni kuwafariji na kuanza kutangaza mkakati mpya ambao utawasaidia wagonjwa kila mara .
akiongea na waandishi wa habari wilayani humo mara baada ya kukabidhi misaada hiyo Mwenyekiti wa Wilaya hiyo Bw Mustapha Mbwambo alisema kuwa misaada hiyo imetolewa kama njia mojawapo ya kutimiza upendo
Mustapha alisema kuwa kwa sasa wameweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa inawasadia wagonjwa na hata wale ambao hawajiwezi kwa misaada mbalimbali ambayo itaweza kuwasaida na kuona kuwa bado serikali na uongozi wa wilaya unawakumbuka.
'ilani ya chama chetu inasema kuwa tuwapenda na tuwajengee mazingira ya kupona wagonjwa sasa sisi hapa Karatu tumeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa kila mara tunatoa msaada lakini pia kuwafariji wagonjwa ambao hawana uwezo na zoezi hili halitakuwa kwenye maazimisho haya ya miaka 37 pekee"aliongeza Mustapha.

Katika hatua nyingine Katibu wa chama hicho ambaye ni Bi Elly Minja alisema kuwa kwa sasa Chama hicho kimeanza kutekeleza ilani ya Chama hicho lakini pia kuanzisha utaratibu maalumu wa kuweza kuwasaidia wananchi kwenye masuala ya msingi ambayo wakati mwingine yanachangia sana umaskini .
Alifafanua kuwa kwa mikakati ambayo inalenga kwenye masuala ya msingi yatachangia kwa kiwango kikubwa sana historia ya mji huo wa Karatu ambao kwa sasa bado unahitaji nguvu kubwa sana ya chama hicho.
"leo tumeweza kufanya mambo mbalimbali ya kichama lakini pia tumeweka malengo ya kuhamkikisha kuwa hata ilani ya chama inatekelezwa kwani kama ikifanikiwa basi itaweza kuwasaidia sana wananchi wa hapa kwetu na hivyo hata kwa mkoa wa arusha nako historia ikiwemo ya umaskini itabadilika sana"aliongeza Bi Minja.

Wakati huo huo akiongea na wananchi wa wilaya hiyo  kwenye viwanja vya Mazingira Bora Mgeni Rasmi kwenye maazimisho hayo, Daniel Awaki ambaye ni Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama hicho kwenye Wilaya hiyo ya Karatu alisema kuwa toka kuanzishwa kwa chama hicho miaka 37 iliyopitwa kuna mabadiliko makubwa sana na mabadiliko hayo hayapaswi kupuuzwa wala kuzomewa na mtu yeyoete.
"tujiulieze kwa sasa ukitoka Arusha mpaka hapa unatumia muda gani na hapo awali ilikuwaje, na wala sio kwenye sekta hiyo pekee bali hata kwenye sekta nyingine za msingi sasa mafanikio kama haya hatupaswi kuyapuuza hata kidogo"aliongeza Awaki.
mwisho

No comments:

Post a Comment