Thursday, January 30, 2014

UKOSEFU WA VYOO WASABABISHA WANAFUNZI ZAIDI YA 300 KUJISAIDIA VICHAKANI

UKOSEFU WA VYOO WASABABISHA WANAFUNZI ZAIDI YA 300 KUJISAIDIA VICHAKANI

ZAIDI ya wanafunzi 300 kutoka katika shule ya msingi Engatani iliopo Kata ya MakibaWilayani Meru Mkoani Arusha wapo hatarini kupata magonjwa ya mlipuko kutokana na kuwa shule hiyo haina vyoo na hivyo wanafunzi wa shule hiyo wanalazimika kujisaidia kwenye vichaka.

Aidha tatizo hilo la ukosefu wa vyoo katika shule hiyo umedumu kwa miaka miwili sasa mara baada ya mvua kubwa kufukia matundu ya vyoo katika shule hiyo.

Akiongea na “majira “shuleni hapo mapema jana Mkuu wa shule hiyo Adamu Kapaya alisema kuwa shule hiyo haina vyoo kabisa na hivyo wanafunzi wanapojisikia kujisaidia wanalazmika kwenda kwenye vichaka au kwenye mazingira ambayo yamejificha kwaajili ya kuweza kujisaidia

Alidai tatizo hilo limeanza mwaka 2012 ambapo mvua kubwa ya masika ilionyesha iliweza kuziba matundu ya vyoo na hivyo kusababisha kutitia kwa vyoo hivyo na mpaka sasa hakuna huduma ya vyoo hali ambayo imesababisha madhara makubwa sana kutokea katika shule hiyo.

“baada ya kuona kuwa mvua zimesababisha shule yetu kukosa vyoo niliandika barua kwa mkurugenzi ambapo naye alihaidi kushugulikia tatizo hili na kwa uongozi wa serikali ya kijiji nlakini mpaka sasa hali ndio kama hii hakuna choo wanafunzi wanakimbilia zaidi kwenye Vichaka”alisema Adamu

Pia aliongeza kutokana na hali hiyo imesababisha hata mazingira ya shule kuwa machafu sana pamoja na kuwepo kwa hewa chafu kutokana na vinyesi ambavyo vimezagaa kwenye mazingira ya shule hiyo na pembezoni mwa shule hiyo hivyo jitiada za haraka sana zinatakiwa kufanyika

Awali diwani Viti maalumu wa Kata hiyo ya Makiba.Bi Joycye Odoko alisema kuwa ukosefu wa choo kwenye shule hiyo umesababishwa na baadhi ya watendaji kukwepa kuombea bajeti shule hiyo kwa lkuwa ipo mpakani mwa wilaya ya Meru hali ambayo inasababisha wanafunzi waishi mazingira magumu sana

Bi Joyce amesema kuwa asilimia kubwa ya wananchi katika eneo hilo ni wafugaaji lakini hawana uwezo kitu ambacho kama wangekuwa na uwezo basi wangeweza kuwasaidia wanafunzi hao

“wananchi wa hapa hawana uwezo ingawaje kwa sasa wameshaweka utartibu hata wa kukusanya mawe , na mchanga ili kuuanza rasmi zoezi hilo japokuwa bado hawataaweza kujenga mpaka kumalizika kwa matundu ya vyoo sassa tunaomba kuwepo  naushirikiano madhubuti baina yetu sisi viongozi ili tuweze kuwasaidia wanafunzi hawa kwani wapo kwwenye hatari kubwa sana ya kuweza kupata magonjwa ya mlipuko hasa kipindupindu”aliongeza Jocye

Akiongelea sakata hilo kwenye baraza la madiwani wa halmahauri ya Meru Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye Goodson Majola alisema kuwa kwa sasa bajeti ya Halmashauri hiyo imelenga kutatua sehemu mbalimbali zenye kero na hivyo pindi watakapopata fedha kutoka Serikali kuu basi wataweza kutatua changamoto mbalimbali

Mwisho

KATA ZA WILAYA YA KARATU ZATAKIWA KUANZISHA MIRADI ILI KUONGEZA UCHUMI KUANZIA NGAZI YA KAYA



Na Queen Lema, KARATU


CHAMA cha mapinduzi Wilaya ya Karatu mkoa wa Arusha kimeagiza uongozi
wa kata zote ndani ya Wilaya hiyo kuhakikisha kuwa inabuni miradi ya
maendeleo ambayo itawasaidia wananchi kuweza kujiongezea kipato lakini
pia kuweza kuondokana na umaskini katika kata zao

Hayo yameelezwa na Katibu wa chama hicho kwa wilaya ya Karatu, Bi Elly
Minja wakati akiongea kwenye harambee ya ujenzi wa jengo la Kitega
uchumi ambalo lipo wilayani humo ambapo pia harambee hiyo ilienda
sanjari na mazoezi mengine mengi ya kuazimisha kuzaliwa kwa CCM hapa
nchini

Bi Elly alisema kuwa kuna haja sasa ya kila kata kuhakikisha kuwa
inakuwa na miradi tena endelevu ambayo itaweza kuwasaidia wananchi
kuondokana na dhana ya umaskini ambayo ikwa sasa ni tishio kubwa sana
kwenye baadhi ya familia.

Alifafanua kuwa miradi hiyo ambayo inatakiwa kubuniwa na wananchi kwa
kushirikiana na viongozi wa kata mbali na kuweza kuwaokoa wananchi
kwenye suala zima la umaskini lakini pia itachangia sana kuongezeka
kwa uchumi wa wilaya hiyo ya Karatu.

Mbali na uanzishwaji wa miradi kwenye kata zote za Karatu pia alisema
kuwa kwa upande wa Jengo la Kitega uchumi lililopo Karatu nalo
litaweza kuwasiaida sana wananchi katika kuboresha uchumi wao lakini
pia litakuwa na faida sana

"uwepo wa jengo hilo la kitega uchumi hapa Karatu ni ishara kuwa sasa
uchumi wa mji wa karatu utaongezeka sana na utaweza kuwasaidia sana
wananchi wa eneo hili hivyo basi wananchi wanatakiwa watumie fursa
ambazo zipo zaidi na sisi tutaendelea kuwa wabunifu zaidi kwa ajili ya
kuweza kuwasaidia wananchi wetu hususani kwenye suala zima la Uchumi
wao wa kila siku"aliongeza Bi Elly


Aliwataka wananchi wa Wilaya hiyo ya Karatu kuhakikisha kuwa
wanaendelea kutumia vema fursa za  maendeleo ambazo zinatolewa na
chama hicho lakini pia wasikubali kupotoshwa juu ya jitiada ambazo
zinafanywa na baadhi ya watu wasiope4nda maendeleo ya jamii nzima


Hataivyo Harambee hiyo ilienda sanjari na mazoezi mbalimbali kama vile
ya upandaji miti,ufanyaji wa usafi wa mazingira pamoja na matembezi
ikiwa ni maazimisho ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi hapa nchini.

SERIKALI YAJITOSA ARUSHA KWA KULIPA FIDIA


Na Queen Lema, Arusha

SERIKALI imefanikiwa kutoa kiasi cha Bilioni moja na Milioni 750 kama fidia kwa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha mara baada ya kuchukua mradi wa Halmashauri hiyo ujulikao kama Laki Laki kwa ajili ya kujenga miji ya kisasa zaidi.

Akidhibitisha mbele ya kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri mkurugenzi mtendaji Bw Fidelis Lumato alisema kuwa mpaka sasa wameshapokea fidia hiyo ya mradi wa mashamba ya Laki laki ambao ulikuwa chini ya Halmashauri hiyo .

Lumato alisema kuwa pamoja na kuwa mpaka sasa wameshaweza kuachia mradi huo na kutoa kwa Serikali kuu lakini fidia hiyo itasaidia sana kuweza kufanya marekebisho ndani ya Halmashauri hiyo ikiwa ni pamoja na kununua mahitaji ya msingi.

Alidai kuwa fidia hiyo imeweza kurahisisha kazi mbalimbali za halmashauri kwa kuwa yapo mahitaji ya msingi ambayo yalikuwa yanahitajika lakini hapakuwa na jinsi ya kupata fedha kwa ajili ya kununua jambo ambalo wakati mwingine lilikuwa linasababisha malengo kukwama.

Aidha alitaja vitu ambavyo vitaweza kununuliwa kutokana na fidia hiyo kuwa ni pamoja na Gari kwa ajili ya matumizi ya shule za sekondari katika Halmashauri hiyo,tipper  kwa ajili ya shuguli za ujenzi ambapo pia nalo litachangia mapato ya halmashauri hiyo.

Vitu vingine ambavyo vitafanyika kutokana na fidia hiyo ni pamoja na ukarabati wa jengo la kisasa la Halmashuri hiyo ambalo bado halijaweza kukamilika rasmi kwa ajili ya matumizi ya Halmashauri hiyo.

“tunashukuru mungu serikali kutupa fidia ya mradi wa mashamba ya Lakilaki kwani kwa kipindi cha mwaka huu tutafanya vitu vingi na tunaimani kabisa hata mapato nayo yataweza kuongezeka zaidi na hivyo kuwasaidia hata wananchi wenyewe”aliongeza Lumato.

Awali Kaimu Mweka hazina wa Halmashauri hiyo ambaye ni bw Munguabella Kakulima alidai kuwa kwa sasa Halmashauri hiyo imeweka mikakati mbalimbali ya kuweza kuongeza vyanzo vya mapato kwani mpaka sasa kuna tofauti kubwa sana ya ongezeko la mapato katika Halmashauri hiyo ya Arusha Vijijini .

Kakulima alidai kuwa hapo awali waliaanza na mapato ya Milioni 400 lakini mpaka sasa wameweza kufikia ukusanyaji wa mapato wa zaidi ya Bilioni 2 jambo ambalo lengo lake ni kuhakikisha kuwa Halmashauri hiyo inaepukana na tabia ya kuwa tegemezi.

MWISHO.

DC AWATAKA MADIWANI KULIMA MASHAMBA YA MIFANO NA KUACHA KUONGEA BILA KUWA NA USHAHIDI WOWOTE WA KILIMO KWANZA



NaMWANDISHI WETU

MKUU wa wilaya ya Arumeru Munasa Nyirembe amewataka madiwani katika halmashauri ya Arusha Vijijini kuhakikisha kuwa wanakuwa wakulima na wafugaji wazuri ili waweze kuwa mfano wa kuigwa na jamii .
Hataivyo mbali na kuwa na mashamba lakini pia hata mifugo ya kufuga pia wanatakiwa kuunga mkono kauli ya kilimo kwanza kwa matendo na wala sio maneno kama ilivyozoeleka kwa baadhi ya viongozi wa kisiasa.

Munasa aliyasema hayo mapema jana wakati akiongea na madiwani katika baraza la madiwani ambalo lilifanyika jana katika halmashauri hiyo .

Alisema kuwa kudai na kusisitiza matumizi ya Kilimo kwanza pekee kwa njia ya mdomo bado hayatoshi kwani kwa sasa kinachohitajika zaidi ni vitendo na wala sio maneno ambayo wakati mwingine hayatekelezwi.

Aliendelea kwa kusema kuwa ili kuweza kuunga mkono kauli hiyo ya Kilimo kwanza ni lazima hata viongozi wenyewe wahakikishe kuwa wanaaanzan kulima lakini hata kufuga kama mfano ikiwa ni jitiaada zaidi za kuongeza na kuimarisha kilimo kwanza.

"inasikitisha sana kama sisi Madiwani hata wakuu wa wilaya tutasimama na kudai kuwa kilimo kwanza kinatakiwa kutekelezwa kwenye maeneo yetu alafu sisi hatuna hata shamba moja la mfano itakuwa ni aibu tupu ni lazima sasa tuanze kulima 'aliongeza zaidi Munasa.

Pia alidai kuwa kama madiwani wa Halmashauri hiyo ya Arusha Vijijini watawea kuweka utaratibu huo wa kulima basi itaweza kuwa kazi raisi sana ya kuweza kusisitiza kilimo kwanza kwani wananchi wataona umuhimu wa kulima lakini kufuga kwa kutumia mbinu za kisasa zaidi.


Alimalizia kwa kusema kuwa ili kilimo kwanza kiweze kuendelea ni lazima kuwepo na ushahidi kuanzia kwa viongozi wa aina zote lakini pia kuwepo na moyo wa uzalendo ambao utalenga kufanikisha zaidi sera za kilimo kwanza.

MWISHO

UJIO WA HELKOPTA YA CHADEMA ARUSHA WAZUA BALAA KWA CCM

Na Mwandishi wetu, Arusha

Chama cha mapinduzi (CCM)kimesema kuwa kinashangazwa na kitendo cha chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema)kutumia Helikpota kwenye chaguzi zake huku kikidai kuwa ni mkombozi wa wananchi jambo ambalo ni kujitafutia sifa na umaarufu pekee  kwa wananchi.
Hayo yameelezwa na Naibu Katibu mkuu wa CCM ambaye pia ni Naibu waziri wa fedha Mwigulu Nchemba wakati akifungua rasmi kampeni za  udiwani katika kata ya sombetini  mapema jana.
Mwigulu alisema kuwa CCM inashangaa sana Chadema kutumia Helikpota kwenye chaguzi nyingi hapa nchini jambo ambalo wanaonesha wazi kuwa wanatumia gharama kubwa kwa ajili ya kuongeza sifa kwani gharama ambazo zinatumika hadi kumalizika kwa kampeni ni zaidi ya Milioni 200.
Alisema kuwa Gharama ambayo inatumika kwenye uendeshaji wa Helkopta ni gharama ambayo ingeweza kuwasaidia wanachama  wao lakini hata matumizi mbalimbali ya chama hicho ambacho bado kinaonekana kukabiliwa na changamoto nyingi sana
Pia aliwataka wananchi kuhakikisha kuwa kamwe hawatumiki kwenye siasa za sifa na ushahbiki kwani siasa hizo wakati mwingine zinasababisha hata vifo vya watu ambao hawana hatia ya kufa ovyo
Awali Mgombea Udiwani katika kata hiyo ya Sombetini kwa tiketi ya CCM alisema Bw David Mollel alisema kuwa ana mikakati mingi sana ya kuhakikisha kuwa anasaidia kata hiyo endapo kama atapata ridhaa ya kuongoza rasmi kama diwani
David alisema kuwa changamoto ambazo atahakikisha kuwa ameweza kuzitatua ni pamoja na urekebishaji wa barabara, uboreshaji wa masoko, kna uimarishaji wa vikundi vya wanawake na jamii kwa ujumla.
MWISHO

MANYARA WAPEWA JEZI

Na GLADNESS MUSHI, Manyara

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara, Mohamed Omary Farah, amegawa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh600,000 kwa timu mbili za soka za Mrara FC na Waangwaray FC za kata ya Babati.
 
Akigawa vifaa hivyo jana kwenye uwanja wa Mrara uliopo mjini Babati, Farah ambaye pia ni Diwani wa kata ya Babati alisema lengo la kugawa vifaa hivyo ni kuhakikisha sekta ya michezo inapiga hatua katika eneo hilo.
 
Alisema anatoa msaada huo wa vifaa vya michezo kwa lengo la kuwaendeleza ambapo timu hizo mbili zilipatiwa kila moja seti moja ya sare za michezo ikiwemo tisheti, bukta na soksi pamoja na mpira mmoja.
 
Alisema kupitia michezo vijana wataweza kujinufaisha kwani hivi sasa michezo ni ajira na pia wataweza kujiweka pembeni na mambo mabaya ikiwemo tabia za uhuni na uvutaji dawa za kulevya.
 
Alisema atahakikisha anakuwa nao sambamba katika michezo kwenye kuwaunga mkono ili timu hizo ziweze kufika madaraja ya juu na kuzileta timu kubwa kwenye mji huo wa Babati.
 
Hata hivyo, mwakilishi wa timu ya Mrara FC Gerald Romly akitoa shukrani kwa niaba ya timu hizo alisema watatumia msaada huo wa vifaa vya michezo kwa kuzitumia ipasavyo kwa ajili ya lengo la kufanikisha michezo.
 
Romly alimshukuru Farah kwa kuwapa msaada huo wa michezo na kuwaomba viongozi wengine kuiga mfano wake, kwani ameonyesha moyo na kujali michezo inayofanywa na vijana wa eneo hilo.
 
MWISHO.

WASOMI VYUO VIKUU ARUSHA WATAKA SERIKALI KUWEKA MTAALA WA MABADILIKO YA TABIA NCHI



NA MWANDISHI WETU, ARUSHA

SERIKALI imeshauriwa kuhakikisha kuwa inaweka mtaala wa mabadiliko ya tabia ya nchi kuanzia ngazi ya shule za msingi ili kuweza kukabiliana na majanga mbalimbali ambayo yanaikumbaa nchi ya Tanzania lakini pia ulimwengu mzima kwa sasa.

Kauli hiyo imetolewa na Bw Peter Mroso ambaye ni Mwenyekiti wa Klabu ya Green Social education(GRESOE) kutoka katika chuo kikuu cha Mt Meru wakati akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wa chuo hicho katika mdahalo wa wanafunzi wa vyuo vikuu Arusha uliofanyika chuoni hapo mapema jana.

Mroso alisema kuwa kwa sasa asilimia kubwa ya wasomi wanafanya kujisomea mambo mbalimbali ambayo yanahusu mabadliko tabia nchi ingawaje kwa sasa nchi inateketea kutokana na majanga hayo hivyo kuna umuhimu mkubwa sana wa kuwepo na mitaala ambayo inahusu mabadiliko tabia Nchi

Aliendelea kwa kusema kuwa endapo kama mitaala ya Tanzania ingeweza kuwa na somo la mabadiliko ya tabia ya nchi basi hata wanafunzi wenyewe wangweza kuwa mabalozi wazuri sana wa masuala hayo ya mabadiliko tabia ya nchi

Amebainisha kuwa njia hiyo ya kuongeza somo la mabadiliko ya tabia ya nchi litaweza kuifanya Tanzania kuepukana na majanga yanayotokana na mabadiliko ya tabia nchi na hivyo kuweza kurudisha hali kama ilivyokuwa hapo mwanzo


Mbali na hayo alidai kuwa nayo serikali inatakiwa kuhakikisha kuwa inaweka mikakati mbalimbali ya kuweza kuwasaidia wananchi wake kwani tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa asilimia kubwa ya wananchi bado hawajajua vema masuala ya mabadiliko tabia nchi


Alimalizia kwa kuwataka nao wasomi kutoka katika vyuo vikuu mbalimbali kuweza kujiweka utaratibuw a kufanya midhalo lakini kuelimisha umma juu ya hatua ambazo zinaweza kutumika ili kupambana na mabadiliko tabia nchi ambayo wakati mwingine ndiyo chanzo cha umaskini hata kwenye vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini.

Mwisho

Saturday, January 4, 2014

MWILI WA WAZIRI MGIMWA WAWASILI NCHINI

PICHANI NI MWILI WA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA DKT WILLIAM MGIMWA UKIWA UMEWASILI NCHINI BAADA YA KULETWA NA NDEGE YA KENYA
 

KIJANA MMOJA AFUKIWA NA KIFUSI,ASKARI WATATU WAJERULIWA KWENYE MAPAMBANO DHIDI YAO NA RAIA KWENYE MKESHA WA MWAKA MPYA




Na Gladness Mushi, Arusha


KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida kijana mmoja aliyetambulika kwa jina
la Joseph Solomon Mkazi wa Terrat Kwa Muorombo jijini Arusha amefariki
dunia mara baada ya kuangukiwa na kifusi cha moramu katika machimbo ya
Terrat

Akiongea na waandishi wa habari mapema leo kamanda wa polisi mkoa wa
Arusha Liberatus sabas alisema kuwa tukio hilo lilitokea leo (Jana}
majira ya saa tatu na nusu za asubuhi huko Terrat

Alidai kuwa marehemu huyo alifikwa na mauti wakati akiwa anajaribu
kukata kifusi kwa kutumia jembe la kulima ambapo pia wakati anakata
kifusi hicho Lori la kubebea mchanga lilikuja kwa nyuma na kasha
kuangusha kifusi kwa haraka

Kamanda Sabasi alifafanua kuwa wakati Lori hilo linaegeshwa ghafla
liliporomoa kifusi hicho ambacho klilimfukia kijana huyo aliyekuwa
anachimba kwa kutimia jembe na kisha kufariki dunia papo hapo



Aliendelea kwa kusema kuwa mara baada ya dereva huyo wa lori kuona
kuwa kifusi kimeanguka ndani ya machimbo hayo aliamua kugeuza gari na
kisha kukimbia huku akiwa ametelekeza mwili wa kijana huyo



“alipoona kuwa ame[egesha gari vibaya na kusababisha mauti alikimbia
lakini wasamaria wema waliweza kuokoa mwili huo ingtawaje mpaka sasa
tunamtafuta dereva wa lori hilo kwani hata namba ya gari nayo bado
hatujaweza kuijua ila jitiada za haraka zinafanyika’aliongeza Kamanda
Sabasi



Pia alidai kuwa wamiliki wa machimbo ya kuchimba Moramu ndani ya mkoa
wa Arusha wanatakiwa kuwa makini sana lakini pia hata wachimbaji ,
madereva nao wanatakiwa kuchukua tahadhari juu ya kazi hiyo kwani
wakati mwingine uzembe unachangia sana vifo visivyo na hatia.



Wakati huo huo Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha inawashikilia vijana
wanne wakazi wa Wilaya ya Meru kwa kosa la kusababishia askari polisi
majeraha pamoja na raia wema kwenye mkesha wa mwaka mpya

Sabasi alisema kuwa wanaoshililiwa ni pamoja na Selemani
Khamisi,Patrick Richard,Jabu Yasini,pamoja nha Khamisi Juma wote
wakazi wa Meru ambapo siku ya December 31 mwaka jana katika eneo la
Ngarasero Usariver,vijana hao waliweza kuongoza kundi kubwa la
wananchi katika kupingana na Serikali dhdii ya kusherkea kwa amani na
utulivu mwaka mpya

Alidai kuwa askari waliokuwa doria katika maeneo hayo walilazimika
kupambana na vijana hao lakini hawakuskia kwa kuwa tayari walikuwa
wameshawasha moto na kuhamasiaha zaidi vurugu jambo ambalo ni kinyume
cha sheria



“wakati polisi wanapambana kutuliza vurugu kundi kubwa la watu
wakiongozwa na vijana hawa walianza kuwarushia mawe polisi na kufanya
fujo kali ambazo pia zilisababisha askari weru kujeruliwa vibaya
sana”alifafanua hivyo kamanda Sabasi



Aidha aliwataja askari walijeruliwa vibaya kuwa ni pamoja na Mkaguzi
msaidizi wa polisi ambaye ni Athumani,Askari namba G 3475
D/CRamadhani,pamoja na askari mgambo ambaye ana namba 97658 Jacob
wakati kwa upande wa Raia ni Aneth Baltazar,Mary Kwayu ambapo pia
Majerui  wote  wamelazwa katika hospitali ya West Meru kwa ajili ya
matibabu



                MWISHO