Monday, December 19, 2011

WENYE WIVU NDIO CHANZO KIKUU CHA MASENGENYO- ASKOFU HOTAY


Baadhi ya wakristo wenye wivu wametakiwa kuacha tabia hiyo kwa kuwa ni chanzo mojawapo cha kuzalisha mawazo ya mtu baki ndani ya mioyo ya watu hali ambayo kwa upande mwingine inazaa dhambi ya wivu

Mtu anapokuwa na tabia ya wivu ni lazima kwanza aweze  kuwa na tabia ya kutopendena kati ya mtu na mtu na hali hiyo ndiyo pia inayozaa matatizo makubwa sana ndani ya jamii

Hayo yamebainishwa mjini hapa katika kanisa la Anglican  St James kaloleni na askofu wa kanisa hilo bw Stanley Hotay wakati akiongea na waumini wa kanisa hilo mapema wiki hii katika ibada ya kuwabariki watoto

Askofu Hotay alisema kuwa ni vibaya sana kama mkristo aliye hai akiwa na tabia ya masengenyo ambayo ni mtoto wa wivu kwa kuwa hali hiyo ni chukizo kubwa sana mbele za mungu.

Aliongeza kuwa ndani ya dunia ya sasa hakuna kitu chochote kile ambacho kitaweza kufanyika na kufanikiwa kama mkristo atakuwa na tabia za wivu kwa kuwa Mungu ndiye anayegawa vitu.

“hii tabia ya wivu kimsingi imetambaa miongoni mwa watu sana unakuta mtu anafikiria mambo ya mwezake na anacha kufikiria mambo yake sasa kwa hali hii kwa nini shetani asiwe ni kikwazo kwetu jamani nawasihii sana achaneni na dhambi hiyo ya wivu rudini katika utukufu wa bwana”alisema Askofu Hotay

Pia katika hatua nyingine alisema kuwa kamwe wivu hauna nafasi katika maisha ya mwanadamu endapo kama mwanadamu atajiwekea utaratibu wa kusikiliza na kuongozwa na sauti ya roho mtakatifu

Alibainisha kuwa endapo wakristo wote watakuwa na tabia ya kumtumia zaidi roho mtakatifu katika mambo yao mbalimbali ni wazi kuwa roho ambazo kwa sasa zinatembea kwa baadhi ya watu zitaweza kufa kabisa .

Hataivyo katika ibada hiyo ambayo iliweza kuwakusanya wakristo wengi sana iliweza kuwa na manufaa makubwa sana kutokana na  kuwepo kwa mambo mbalimbali wakiwemo walemavu wa ngozi(ALBINO) pamoja na kubariki watoto 80.

MWISHO
CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA

0758907891

ARUSHA

OLE WENU NINYI WACHUNGAJI NA MAASKOFU MNAOPINGA HUDUMA CHANGA



 Wito umetolewa kwa baadhi ya wachungaji wakubwa na wenye majina makubwa hapa nchini kuhakikisha kuwa wanaachana na tabia ya kudharau huduma ambazo ni ndogo na changa kwa kuwa mungu haangalii zaidi ukubwa wa jengo bali anaangaliwa wingi wa watu wanaomcha katika maisha yake

Hayo yamesemwa na askofu wa kanisa la international Chastmatic church,(ZION TEMPLE)Bw fitiaely urio katika ibada ya kuwaweka wakfu  sanjari na kuwaweka kazini rasmi wachungaji  nane wa kanisa hilo lilopo katika maeneo ya Ungalmtd jijini hapa.

Askofu Fitiaely  alisema kuwa ndani ya jamii ya sasa bado kuna baadhi ya wachungaji ambao mara nyingi wamekuwa wakidharau na kukataa huduma mbalimbali za wenzao kwa kuwa ni changa

Alibhainisha kuwa hali hiyo si njema na ni chukizo kubbwa sana mbele za mungu kwa kuwa mungu hana vigezo kama walivyonavyo baadhi ya wanadamu hapa duniani.

“ukiangalia utakuta maskini mchungaji kaamua kuanzisha kanisa lake na huduma yake lakini kwa kuwa mchungaji wa jirani yeye anawa umini wengi zaidi anawaacha waumini wake kuwalea kiroho na kimwili alafu eti anaangalia zaidi ile huduma changa sasa kwa maana hiyo kanisa la leo linakwenda wapi jamani’aliwahoji waumini

Katika hatua nyingine mtumishi huyo alienda mbali zaidi na kusema kuwa nao wachungaji ambao wanakuwa na waumuini wachache miaka yote nao ni wakuuliza maswali kwa kuwa miongoni mwao kutakuwa na kasoro

Alisema kuwa wanapswa kukumbuka biblia ilivyosema na kuahidi kuwa tunatakiwa kuwaleta watu wengi kwa yesu kwa maana kama mchungaji hana waumini miaka yote ni wazi kuwa anakiuka sharti hilo.

‘pamoja na kuwa wachungaji wanawakataa wenye huduma changa lakini sisi kama sisi tunatakiwa kujiuliza ina maana hata kwa mara moja huyu mchungaji hashawishiki hata kumleta mtu kwa yesu au yupo kivingine ‘alisema mtumishi huyo

Pia alianisha kuwa nao wachungaji  na wakuu mbalimbali wa idara wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanaachana na tabia ya kuweka mbele zaidi maslahi katika huduma zao kwa kuwa hayo maslahi ndiyo chanzo mojawapo cha kukataliwa na jamii

Alisiisitiza kuwa kwa mtumishi ambaye ameitwa na mungu anapaswa kujua kuwa malipo yake yapo mbinguni na wala sio hapa duaniani ambapo kuna fedha na kwa njia ya kudai malipo kwa ajili ya ukombozi wa watu ndiyo kichocheo mojawapo cha kujiunganisha na falme nyinginezo

MWISHO 

CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA
O758907891

ARUSHA 

TRA ARUSHA YAFANIKIWA KUWAFARIJI WATOTO YATIMA




Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoani Arusha imetoa misaada yenye thamani ya zaidi  sh.miloni moja na nusu kwa vituo vya watoto yatima  ikiwa ni kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya mlipa kodi.

Akikabidhi misaada hiyo meneja mkoa wa Arusha Evaristo Kileva alisema kuwa misaada hiyo ni njia mojawapo ya kuhakikisha kuwa mamlaka inatoa msaada kidogo ili kuwapa nguvu wanajamii wenye mioyo ya kufanya kazi.

Kileva alisema kuwa mamlaka inatambua mchango wa walipa kodi hivyo iliona ni muhimu wiki  ya maadhimisho ya mlipa kodi iwatembelee watoto  yatima kwa kuwapatia misaada mbalimbali ili iweze kuwasaidia na kutambua kuwa mamlaka ipo pamoja nao.

Aidha ameongeza kuwa watoto yatima ni taifa la kesho hivyo wakilelewa katika mazingira mazuri ikiwa ni pamoja na kupata chakula,elimu bora, malazi na mavazi  basi ni wazi wataongeza juhudi katika masomo yao hali itakayowezesha taifa la kesho kuwa lenye jamii iliyoelimika.

Hata hivyo amewataka watanzania,mashirika na taasisi mbalimbali kuwaunga mkono vituo vya watoto yatima kwa kuchangia hata kidogo walichonacho kwani watoto hao wanahaki sawa ya kupata elimu bora kama watoto wengine.

Naye mkurugenzi wa kituo cha Nora Children Care Trust ambacho ni miongoni mwa kituo kilichopatiwa msaada bi.Nora Anthon alisema kuwa changamoto kubwa ni pamoja na ukosefu wa  kuwapatia watoto elimu,chakula,matibabu na usafiri  kutokana na kituo kukosa mradi.

Hata hivyo misaada  iliotolewa ni pamoja na mchele,maharagwe,unga wa lishe,unga wa sembe,maziwa,sukari,madaftari,mashuka,mablanketi,sweta za shule,mafuta ya kupikia,sabuni,na kalamu.

Vituo vilivyopatiwa misaada ni pamoja na nora children care kilichopo eneo la makumira nje kidogo ya jiji la Arusha na kituo cha yatima cha The Christian women emancipation organization kilichopo sinoni ungalimited.

Mwisho……

CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA

0758907891

ARUSHA

Friday, December 2, 2011

NYIE MNAOTOA MISAADA KAMWE MSIIKUMBUKE

Mchungaji Mama furaha Simtenda kutoka Tanga amewataka wakristo
mbalimbali hapa nchini kuhakikisha kuwa kamwe wanapotoa msaada
mbalimbali kamwe hawakumbuki misaada au sadaka hizo kwa kuwa kwa njia
ya kukumbuka ni wazi kuwa wanajionesha kwamba hawajatoa kwa moyo.

Mama furaha aliyasema hayo katika kanisa la Anglican st James wakati
alipokuwa akifundisha semina  kwa waumini na wakristo mbalimbali juu
ya umuimu wa kutoa kwa moyo

Alisema kuwa ustaarabu ambao upo kwenye makanisa ndio unaotakiwa
kuwepo kwenye utoaji wa misaada mbalimbali kwa kuwa mungu anapenda
mtoaji asikumbuke kamwe ambacho amekitoa

“unakuta mtu anampa mtu hata nguo alafu akisha muona amependeza bila
kujali anaanza kusema kuwa ni mimi ndiye niliyempa sasa makanisani
mlishaona mtu akitoa zaka anaongea inakuwaje misaada inakuimbukwa ,huo
sio utoaji”aliongeza Mama furaha

Pia alisema kuwa kila mkristo anatakiwa kuhakikkisha kuwa analipa
garama mbalimbali ambazo zilitolewa na bwana yesu mslabani kwa kuwa
yesu alilipa garama za kila kizazi bila kujali itikadi za dini wala
rangi

Aliongeza kuwa kupitia garama ambazo zimelipwa na bwana yesu kila
mwenye mwili anatakiwa kuwa mna moyo wa kujitoa sana kwa kuwa kwa sasa
bado wapo baadhi ya watu ambao hawajitoi hata katika machangizo
mbalimbali hali ambayo si sahihi mbele za mungu.

Alisema kuwa ili uweze kutoa michango mbalimbali ndani ya makanisa
unatakiwa kuhakikisha kuwa unakuwa na tabia ya imani kwa kuwa suala
zima la utoaji lina sanjari na imani ‘ambayo ndiyo msingi imara.

“kama hauna imani ni wazi kuwa kila utakalo kuwa unalifanya ni bure ni
sawa tu  na umesogeza kitu mbele yako lakini kama una imani basi
utaweza kupokea kile lunachokitaka kwa maana hiyo nawasihi muwe na
imani kwa kuwa imanik ndio msingi mkuu”aliongeza Mama furaha


Hataivyo aliwataka wakristo kuhalkikisha kuwa wanatoa bila kuangalia
mifukoni mwao kilichobakia kwa kuwa biblia imeonesha wazi  mungu akiwa
upande wa mwanadamu hakuna ambaye atakuwa juu zaidi kwa maana hiyo
kila kitu kinawezekana kwa mungu.

CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA
ARUSHA
0758907891