Saturday, October 26, 2013
NYUMBA ZA ASKARI ZIMA MOTO ARUSHA ZAKABILIWA NA UCHAKAVU ULIODUMU KWA ZAIDI YA MIAKA 50
Na Queen Lema, Arusha.
Jeshi la zima moto na ukoaji mkoa wa Arusha linakabiliwa na changamoto
ya uchakavu wa nyumba uliodumu kwa miaka zaidi ya 50 ambapo pia
uchakavu huo wa nyumba unaenda sanajari na uahba wa Vyoo hali ambayo
inasababisha ongezeko la magonjwa ya Malaria kutokana na nyumba hizo
kugeuka kuwa makazi ya Mbu.
Aidha nyumba hizo zilijengwa mwaka 1954 ambapo mpaka sasa hazijaweza
kufanyiwa marekebisho ya aina yoyote ile hali ambayo inasababisha
nyumba hizo kugeuka magofu.
Hayo yamelezwa na Andrew James Mbate ambaye ni kamanda Zima moto na
uokoaji mkoa wa Arusha wakati akiongea na wafanyakazi wa jeshi hilo
mara baada ya kumuaga aliyekuwa kamanda wa jeshi hilo Bw Jesward
Ikonko mapema jana.
Kamanda Andrew alisema kuwa nyumba hizo za jeshi zilijengwa miaka
mingi iliyopita lakini toka kujengwa kwake mwaka 1954 mpaka sasa
hazijaweza kufanyiwa marekebisho ya aina yoyote ile jambo ambalo
linasababisha wafanyakazi pamoja na familia zao ziweze kuishi maisha
ya kuugua kila mara.
“tunaweza kusema kuwa nyumba hizi zimegeuka nyumba za mbu kwani kwa
juu hazijaweza kuzibwa na baridi yote inapita lakini pia hata kwa juu
kwa kuwa kuna uwazi mkubwa sana unasababisha mbu kukaa kama nyumbani
kwani sasa hali hiii kwa kweli inasababisha wafanyakazi wetu washindwe
kufanya kazi zao kwa kufuraia makazi’aliongeza hivyo.
Pia alisema kuwa mbali na nyumba hizo kugeuka chakavu sana lakini pia
hata suala la vyoo navyo ni chakavu kwa kiwango cha hali ya juu jambo
ambalo ni hatari kwa afya za watumiaji
“tunaweza kujiuliza kuwa choo kilichojengwa mwaka 1954 mpaka sasa
kitakuwaje na kinatumiwa na familia nyingi je kwa hali hii wafanyakazi
wataweza kufuraia maisha au ndo wataboreka “alihoji Kamanda huyo.
Kutokana na hali hiyo alisema kuwa ni vema kama mchakati wa nyumba
hizo za watumishi sasa zikageukia upande wa Wizara kutoka katika
mikono ya Jiji la Arusha kwani kama zitakuwa chini ya wizara zitaweza
kupata marekebisho makubwa ambayo yataongeza utendaji kazi mzuri wa
wafanyakazi.
Akiongelea suala zima la utendaji kazi wa kikosi hicho cha zima moto
mkoa wa Arusha alisema kuwa mkoa wa Arusha unakabiliwa na tatizo la
ujenzi holela hali ambayo inasababisha wakati mwingine washindwe
kuokoa baadhi ya nyumba ambazo zinateketea kwa Moto hivyo basi ni vema
kama kamati ya mipango miji wakati mwingine ikawa inatoa elimu kwa
wananchi wanaotaka kujenga nyumba zao.
MWISHO
IDADI YA WANAWAKE WABUNGE SADC IMEONGEZEKA
Na Gladness Mushi,Arusha
IDADI ya wabunge wanawake kwenye nchi wanachama wa mabunge ya nchi za
kusini mwa Afrika (SADC) imeongezeka ingawaje kwa Tanzania bado baadhi ya
wanawake wanahofu kubwa ya kushiriki katika chaguzi mbalimbali kutokana na
changamoto zilizopo kwenye jamii
Hayo yameelezwa
na Anna Makinda ambaye ni Spika wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akiongea na vyombo vya habari mapema
leo kuhusiana na mkutano wa 34 wa jukwaa
la Mabunge ya Nchi wanachama wa jumuiya
ya maendeleo kusini mwa Afrika unaotarajiwa kufunguliwa na Makamu wa
Raisi dkt Gharib Bilali mapema jumapili ijayo.
Aidha
Makinda alisema kuwa kuongezeka kwa wabunge wanawake katika mabunge ya SADC
kunatokana na juhudi mablimbali ambazo zinafanywa na jumuiya hiyo hali ambayo
nayo imefanya mabadiliko makubwa sana kwenye baadhi ya nchi.
Alisema kuwa
pamoja na ongezeko kubwa la idadi ya wabunge wanawake katika jumuiya hiyo
lakini kwa Tanzania bado baadhi ya wanawake wanauoga na hofu ya kushiriki
katika chaguzi kuu jambo ambalo wanatakiwa kulipinga.
"hapa
tunaona kuwa hii idadi ya wanawake ni kubwa katika jumuiya hii ya SADC lakini
kupitia ongezeko hili ni muhimu sana kwa wanawake wa Tanzania nao wakahakikisha
kuwa wanajitokeza kwenye chaguzi mbalimbali na kushiriki kwani uwezo wa wao
kuwa wabunge upo na wasiogoope wala kujiwekea udhaifu wa changamoto”aliongeza
Makinda
Wakati huo
huo alidai kuwa wanawake wa Tanzania hawapaswi kukatishana tamaa wao kwa wao na
badala yake wanatakiwa kupena moyo hasa pale wagombea wanawake wanapokutana na
changamoto kubwa ambazo wakati mwingine zinasababisha baadhi yao kukimbia
nafasi za uongozi
Awali
akiongelea mkutano huo wa 34 alisema kuwa Nchi ya Tanzania imepewa nafasi ya
kuwa mwenyeji mkuu wa mkutano huo ambao utaweza kuwashirikisha viongozi wa Mabunge
mbalimbali kutoka SADC na hivyo kupitia mkutano huo wataweza lkujadili mambo
mbalimbali
Makinda alisema
kuwa mkutano huo utaaangalia vitu muhimu kwa nchi wananchama kama vile vigezo vya kusimamia na kutathimini mwenendo
wa chaguzi za nchi wanachama wa jumuiya hiyo.
“Kauli mbiu
ya mkutano huu ni vigezo vya kuendesha
na kutathimini chaguzi kwa nchi za kusini
mwa Afrika hivyo basi hapa tutaweza kuangalia na kukagua hilo hivyo
tutaweza kupata hata majibu ambayo yatasaidia nchi zetu”aliongeza Makinda.
MWISHO
WAFADHILI KUTOKA UJERUMANI WATOA MSAADA WA VITABU WENYE THAMANI YA ZAIDI YA MILIONI 9
WAFADHILI kutoka Ujerumani wamefanikiwa kutoa msaada wa
vitabu venye thamani ya Milioni tisa kwa shule ya sekondari Leguruki iliopo
Wilayani Meru mkoani Arusha kwa lengo la kuongeza ufanisi wa elimu zaidi kwenye
shule hiyo.
Akiongea na wanafunzi shuleni hapo mapema jana mara baada ya
kupokea msaada huo Mjumbe wa kamati ya siasa mkoa wa Arusha John Palangyo
alisema kuwa msaada huo utasaidia sana
shule hiyo ya sekondari ambayo pia ipo chini ya Chama cha mapinduzi.
Palangyo alisema kuwa wafadhili hao wameamua kutoa msaada
huo wa vitabu venye thamani ya milioni tisa lakini ni wajibu wa wanafunzi
kuhakikisha kuwa wanavisoma na kuvifanyia kazi vitabu hivyo kwani vina mitaala
ya nchi ya Tanzania
Pia alsiema kuwa kama
wanafaunzi wa shule ya sekondario yoyote ile hapa nchini watakuwa na tabia ya
kujisomea vitabu mbalimbali basi watachangia kwa kiwango kikubwa uelewa tofauti
na sasa ambapo bado wapo wanafunzi wanaosoma kwa kufundishwa na walimu pekee.
Alibainisha kuwa kuna umuhimu mkubwa sana
wa walimu wenyewe kuhakikisha kuwa wanawasisitiza wanafunzi kujisomea vitabu na
kuachana na tabia ya kujidanganya kuwa hata wasiposoma watakuwa na maisha
mazuri tena yenye mvuto wa hali ya juu jambo ambalo nalo linachangia sana kuongeza idadi ya
wanaofeli katika shule za Sekondari pamoja na Vyuo vikuu hapa nchini
“mimi napenda kuwaambia kuwa msije kuona kuwa watu
wana
maisha mazuri mkadhani kuwa hawakujituma kusoma vizuri shuleni ni lazima
kama mnataka maisha mazuri basi mjitume kusoma kwa bidii
lakini pia msikubali kujiwekea fikra ambazo zinawapotosha kwani hizo
ndizo
zinazochangia ninyi mje kuwa na maisha
mabaya hapo baadae”aliongeza Palangyo
Katika hatua nyingine aliwataka hata walimu kuwatengenezea
wanafunzi mazingira mazuri na kuwapa
motisha wanafunzi hasa kwenye suala zima
la usomaji wa vitabu kwani kwa kufanya hivyo kutaweza kuruhusu walio wengi
kupenda kujisomea vitabu.
Awali mkuu wa shule hiyo ya Leguruki Emanuel Loi alisema
kuwa msaada huo wa Vitabu umekuwa na tija kubwa sana shuleni hapo kwani hapo awali shule
nzima ilikuwa na vitabu 52 na sasa wameweza kufanikiwa kupata vitabu zaidi ya
elfu jambo ambalo litaweza kuwanufaisha wanafunzi shuleni hapo
Alimaliiza kwa kusema kuwa hata wazazi nao wana jukumu kubwa
sana la
kuhakikisha shule za sekondari zinakuwa na Vitabu vya kutosha ili kuweza
kuharakisha maendeleo ya elimu
MSIWAACHIE WATOTO UHURU WA UTANDAWAZI NDIO CHANZO CHA KUFELI
Na gadness, Arusha
IMEELEZWA kuwa tabia ya wazazi kuwaachia watoto uhuru wa
utandawazi hasa simu za mikononi kwa muda mrefu ndio chanzo kikubwa cha
mdonodko wa elimu kwa nchi ya Tanzania
kwani kwa sasa wapo baadhi ya wanafunzi ambao wanatumia muda mrefu sana kwenye utandawazi
kuliko kwenye elimu
Kwa sasa hata mitandao ya kijamii ambayo ipo inatumiwa
wakati mwingine vibaya na wanafunzi hali ambayo wazazi wanatakiwa kuchukulia
tahadhari tena kwa haraka sana.
Hayo yameelezwa na Askofu Erick Mukwenda wakati akiongea na
wazazi pamoja na walezi wa wanafunzi wa darasa la saba kwenye shule ya
Maranatha iliopo jijini Arusha mapema jana katika maafali ya sita ya shule
hiyo.
Askofu huyo alisema kuwa maana halisi ya utandawazi wakati
mwingine imegeuzwa kabisa na wanafunzi na hivyo wengi wanadhubutu kuwekeza huko
kuliko kuwekeza zaidi kwenye masomo jambo ambalo ni hatari sana
Alisema kuwa ili kuikwepesha jamii na tabia hiyo ni lazima
kwanza wazazi waangalie suala hilo kwa mapana
zaidi kwani wakati mwingine watawakemea
watoto baasi wataogopa na hawatajihusisha sana
na mitandao hiyo au utandawazi
Pia aliongeza nao wazazi wanatakiwa kuhakikisha kuwa
wanaepukana na tabia ya kufikiria zaidi ada kuliko kufikiria malezi ya watoto
kwani kwa sasa walimu pekee ndio wanaoachia suala zima la malezi jambo ambalo
wakati mwingine linakuwa gumu sana
“kama tunataka maendeleo ya elimu kwa nchi ya Tanzania ni
lazima kwanza tuhakikishe kuwa tunashirikiana kwenye malezi kwani malezi ya
wanafunzi sio ada bali hata maadili hivyo basi wazazi sasa mnatakiwa
kubadilika”aliongeza Askofu huyo
Katika hatua nyingine aliwataka wazazi pia kuwapa elimu
wanafunzi juu ya matumizi ya simu za mkononi lakini pia kuachana na tabia ya
kuwapa simu pindi wanapokuwa mashuleni kwani pia jambo hilo
pia linachangia sana
wanafunzi kuwazia simu kuliko masomo.
MWISHO
SERIKALI YATAKIWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFUGAJI ILI WASIKONDE WAO NA MIFUGO YAO
|Serikali imetakiwa kuboresha mazingira ya wafugaji wan chi ya
Tanzania pamoja na miundombinu yake kwani kwa sasa wapo baadhi ya
wafugaji ambao hawanufaiki na ufugaji na badala yake wanakonda wao
pamoja na mifugo yao
Hayo yameelezwa Jijini hapa na Naibu waziri wa mawasiliano sayansi na
Teknolojia January Makamba wakati akiongea na wataalamu wa mifugo
Tanzania mapema jana kwenye mkutano wa 36 unaondelea jijini hapa.
Makamba alisema kuwa inaskitisha kuona kuwa wafugaji na mifugo yao
imekondeana kwa kuwa haina mazingira mazuri hivyo kuna umuhimu mkubwa
sana wa Serikali kuwekeza kwenye sekta hiyo ambayo bado inakabiliwa na
changamoto kubwa
Alisisitiza kuwa kama mazingira ya wafugaji wa Tanzania yataweza
kuboreshwa kwa asilimia 100 ni wazi kuwa hata mazao yanayotokana na
mifugo nayo yatakuwa ya hali ya juu sana hivyo kuruhusu kuweza kuingia
hata kwenye soko la dunia.
“katika nchi ya Tanzania wapo baadhi ya wafugaji ambao wanafuga
ilimradi waonekane nao wamefuga sasa hili si jambo jema ni muhimu sana
kwa Serikali kuweza kuboresha mazingira na miundombuni lakini pia
kuweza kuwapa misaada muhimu kwa ajili ya kuhimiza uzalishaji na
ufugaji bora zaidi”aliongeza Makamba
Pia alisema kuwa tabia ya kubaki na idadi ya mifugo hususani ngombe
kwenye takwimu za nchi bado haitoshi na wala haijengi bali Nchi
inatakiwa kuwa na takwimu nzuri sana za uzalishaji na ufugaji bora
kama ilivyo kwa nchi zilizoendelea katika sauala zima la mifugo.
Naye mwenyekiti wa chama cha wataalamu wa mifugo Tanzania Stella
Bitende alisema kuwa bado kuna umuhimu mkubwa sana wa Serikali
kuhakikisha kuwa hata wananchi wa Vijijini nao wanapata huduma za
wataalamu wa mifugo kwani idadi ya wataalumu hao(Maafisa Ugani)ni
ndogo sana ukilinganisha na uitaji
Bitende aliongeza kuwa kama Serikali itaweza kuongeza idadi ya
wataalumu wa ugani hasa katika maeneo hayo ya vijijini basi ufugaji
utaweza kuwanufaisha wananchi wengi sana tofauti na sasa ambapo katika
maeneo ya vijijini bado wanatumia mbinu na njia za zamani sana
Alimalizia kwa kusema kuwa pamoja na kuwa chama hicho kimeweza
kujipanga hasa katika masuala ya tafiti mbalimbali lakini bado zipo
changamoto kubwa kama vile nyenzo za uzalishaji ,ambazo zinawanyima
kufanikiwa katika uzalishaji kwenye sekta ya mifugo.
MWISHO
Wafanyakazi wa hoteli hawana ujuzi na elimu ya kutosha.
IMEELEZWA
kuwa asilimia kubwa ya watanzania wamekuwa
hawapati nafasi mbalimbali za ajira kwenye mahoteli kutokana na wengi
wao kutokuwa na elimu ya kutosha na
hivyo kuchangia wageni kutoka nje ya nchi kupata ajira kwa urahisi .
Aidha hali
hiyo imekuwa ikichangia kwa kiasi kikubwa sana vijana wengi kukosa ajira katika
mahoteli kutokana na wengi wao kutokuwa na elimu ya vitendo na hivyo kuishia kutumia elimu ya
darasani.
Hayo
yalisemwa jana na Meneja wa
programu wa shirikisho la vyama vya
utalii Tanzania (TCT) Fatma Mabrouk alipokuwa akizungumza na wamiliki wa mahoteli
jijini Arusha wakati wa kuutambulisha programu ya mafunzo kazini ambayo itawanufaisha vijana wenye umri
wa miaka 17-25.
Alisema
kuwa, programu hiyo kwa sasa ipo katika hatua ya majaribio kwa miaka miwili ambapo wameanzia jijini Dar
es Saalamu kwa kuzungumza na wamiliki wa
mahoteli kwa lengo la kuitambulisha programu hiyo ili waweze kuitumia kwa
wafanyakazi wao na kuongeza ufanisi na
utendaji kazi zaidi.
Fatma
aliongeza kuwa,programu hiyo itasaidia kuwaongezea wafanyakazi wa mahoteli
ujuzi zaidi katika utendaji kazi wao kwani wengi wao hawana ujuzi huo hali inayochangia wengi wao kushindwa
kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
‘kwa sasa
hivi wengi wao wanajifunza masomo ya darasani kwa asilimia 70 huku makazini
wakitumia asilimia 30 tu, hali ambayo inaadhiri utendaji kazi wao kwa kiasi
kikubwa kutokana na kutumia muda mwingi darasani badala ya makazini’alisema Fatma.
Naye
Mkurugenzi mtendaji wa chama cha mahoteli
Tanzania(HAT) ,alisema kuwa,Lathifa Sykes alisema kuwa,baada ya muda
majaribio kumalizika programu hiyo itapitishwa kuwa sheria na hatimaye kuweza
kutumika katika vyuo mbalimbali vya utalii hapa nchini .
Sykes
aliongeza kuwa,kwa sasa vyuo vingi vya utalii vimekuwa vikitoa elimu hiyo kwa
njia tofauti tofauti na hivyo kupitia programu hii itasaidia kufundisha kitu
kimoja kwa vyuo vyote na hivyo kuwawezesha wanafunzi hao kupata ujuzi
unaohitajika katika soko la hoteli.
Alisema
kuwa,programu hiyo inafadhiliwa na shirika la kazi duniani (ILO) ambapo lengo
halisi ni kuhakikisha kuwa idadi ya wafanyakazi kwenye mahoteli inaongezeka .
Mwisho.
Tuesday, October 1, 2013
MBUNGE LEMA,AFUTIWA MASHITAKA
Na
GLADNESS MUSHI, ARUSHA
Mahakama
ya hakimu mkazi imefuta kesi iliyokuwa inamkabili mbunge wa jimbo la Arusha Goodbless
Lema na kudai kuwa upande wa mashitaka hakuwa na nia ya kuendeleza kesi hiyo.
Aidha
kesi hiyo iliyokuwa inamkabili mbunge huyo ilikuwa ni ya uchochezi katika chuo cha uhasibu Arusha ambapo vurugu
hizo zilisababisha chuo hicho kufungwa.
Pia
kesi hiyo ilipangwa kuanza kusikilizwa leo mbele ya Hakimu Devotha Msofe wa Mahakama ya
Hakimu Mkazi Arusha ili kuweza kuitolea ufafanuzi zaidi.
Hataivyio
mara baada ya hakimu huyo pamoja na Jopo la mawakili kuingia mahakamani hapo,
Wakili wa Serikali Elianenyi Njiro, aliiomba mahakama kesi hiyo ifutwe chini ya
kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, kama
ilivyorekebisha 2002.
Ilidaiwa
mahakamani hapo kuwa upande wa mashitaka uliona hauna haja wala tija ya
kuendelea na kesi hiyo lakini pia ni vema kama kipengele cha sheria
kikaangaliwa zaidi.
Pia
mara baada ya ombi hilo mahakama iliridhia na kudai kuwa kuanzia sasa Mbunge
huyo yupo huru kwa mujibu wa kifungu cha sheria.
Awali
Akisoma maelezo ya awali Julai 10 mwaka huu mahakamani hapo, Wakili wa Serikali
Elianenyi alidai Aprili 24 mwaka huu, Lema akiwa eneo la Freedom Square la IAA
alifanya kosa la uchochezi wa kutenda kosa kinyume na Sheria ya Kanuni ya
Adhabu.
Akifafanua
shtaka hilo, Elianenyi, alidai kuwa Lema aliwaeleza wanafunzi wa chuo hicho
ambao walikuwa wamekusanyika kufuatia kuuawa kwa mwenzao na watu wasiojulikana
kuwa;
Upande
wa mashtaka tayari ulikuwa umewaleta mashahidi watano ambao ni Kamanda wa
Polisi wa Wilaya ya Arusha, Giles Mroto, Naibu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha,
Faraji Kasidi, Inspekta wa Polisi Bernard Nyambalya, Jane Chibuga na Mwadili wa
Wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha, John Joseph Nanyaro.
MWISHO
Subscribe to:
Posts (Atom)