Wednesday, March 5, 2014

MADIWANI 23 MERU WATISHIA KUJIUZULU NA KUKUSANYA KADI ZA CCM NA WANACHAMA WAKE.

MBUNGE WA JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI JOSHUA NASSARI



MADIWANI 23 MERU WATISHIA KUJIUZULU NA KUKUSANYA KADI ZA CCM NA WANACHAMA WAKE.


KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida madiwani 23 kutokaa katika Halmashauri ya Meru mkoa wa Arusha wametishia kujiuzu wote katika nyadhifa zao lakini pia kukusanya kadi zote za chama cha mapinduzi sanjari na kuongoza maelfu ya wananchi kwenda kuchukua ardhi yao ambayo imetekwa kinyemela,endapo kama Halmashauri hiyo haitatoa tamko rasmi dhidi ya migogoro ya mashamba inayoendelea Wilayani Humo.

Aidha pia kadi ambazo zitakusanywa zitaweza kuwekwa chini ya uangalizi maalumu ikiwa ni pamoja na kutojihusisha na kazi yoyote ile ya chama cha mapinduzi ikiwa ni fundisho kwa serikali dhidi ya vigogo wake wa Wizara ya Ardhi ambao wanatumika katika migogoro ya ardhi katika Halmashauri Mbalimbali.

Madiwani hao waliyasema hayo ijumaa iliyopita katika baraza la madiwani lililofanyika katika Halmashauri hiyo ambapo agenda ya migogoro ya ardhi ilifanya baraza hilo kujikuta likiwa linatoa tamko na vitisho vikubwa kwa watumishi wa Halmashauri hiyo.

Akiongea kwa niaba ya madiwani wa Halmashauri hiyo bi Mwanaidi Kimu alisema kuwa wameschoshwa kila siku kujadili agenda za migogoro ya ardhi lakini hakuna utendaji wowte na badala yake wanabaki wakiwa na kumbukumbnu ya vikao katika vichwa vyao hali ambayo kwa sasa imefika mwisho

Akitolea mfano moja yashamba lenye migogoro katika Halmashauri hiyo,shamba la  Madira lililopo katika maeneo ya Seela Singisi ambalo  ni mali halisi ya Halmasahuri hiyo lakini kwa sasa kuna migogoro ambayo inasababishwa na baadhi ya viongozi jambo ambalo wamedai kuwa hawataweza kuvumilia bali wataingia katika vita kwa mara nyingine

“kwa mfano hili shamba la Seela Singisi ni mali ya wananchi wote wa Meru na hadi Raisi ameshaweka saini yake jamani litumike kwa ajili ya matumizi ya kata zote za Meru lakini vigogo wanasema ni mali yao alafu bado tumenyamaza tu haitawezekana tunaachia udiwani alafu htunaingia katika Vita kwa mara nyingine”aliongeza Kimu

Katika hatua nyingine akiongea kwa niaba ya madiwani wanaume ,Wilson Nyitti alisema kuwa hali hiyo imesababisha kila wanpopita walazimke kujikuta wakiwa wanazomewa ovyo na wananchi kwa kuwa wananchi wanafikiri kuwa wao wananufaika na migogoro hiyo ya ardhi

Nyitti alisema wamechoka na hali hiyo ya kudhomewa na kuabishwa mara kwa mara wakati hawausiki na kutokana na hilo sasa wamejipanga kushirikiana na wananchi kurudi kwanye vita kwa mara nyingine kwa ajili ya kuchukua ardhi yao lakini kupigana hata ikiwezekana kabisa.

“hili ni tamko rasmi tunatoa tunataka majibu ya migogoro hii rasmi kama hatupewi itakuwa ni vita baina ya Wameru na hawa wanaojichukulia ardhi kinyemelea, pia itakuwa ni huzuni kubwa kwa CCM  manake kwanza sisi wote hapa tunatokea CCM uzalendo umetushinda kabisa”aliongeza Nyiti

Naye Mwenyekiti wa Halmasahuri hiyo ya Meru, Goodson Majola alisema kuwa tamko hilo la kutaka kujiuzulu kwa madiwani 23 wote wa halmashauri hiyo lipo sawa kabisa kwa kuwa migogoro yote ya ardhi inasababishwa na Viongozi wasio waadilifu kuanzia ngazi ya Halmashauri hadi Wizara

Akiongelea suala la shamba hilo la Madira alisema kuwa Raisi Kikwete tayari ameshatoa ardhi hiyo yenye jumla ya Hekari 360 lakini bado hawajaweza kulitumia kutokana na vitisho ambavyo walikuwa wanavipata kutoka kwa vigogo

“mimi nasema kuwa tutajiuzulu wiki chache zinazokuja baada ya kujiridhisha juu ya maangaiko haya ya ardhi ambayo yamedumu toka karne hadi karne na ninasiistiza kuwa itakuwa ni kilio kwa CCM kwa kuwa wanchama wetu nao tutaweka chini ya ulinzi hadi tutakapowaambia hawatajishugulisha na shuguli yoyote ya chama”alisema Majola.

Majola alisema kuwa kujiuzulu kwao lakini pia kuondoka na wanachama wote wa CCM katika Wilaya hiyo ni uzalendo wao kwa wananchi na hivyo Hata CCM nao hawapaswi kuumia kwa hilo.

Hataivyo Halmashauri hiyo inaoongozwa na madiwani wote wa CCM lakini pia kwa upande wa wapinzani inaongozwa na Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari.

MWISHO

MSIAMBUKIZE VIRUSI KWA MAKUSUDI-RC MULONGO

MKUU WA MKOA WA ARUSHA, MAGESA MULONGO.



mkuu wa mkoa wa Arusha magesa mulongo amewataka baadhi ya wagonjwa
wanaoishi na virusi vya ukimwi kuhakikisha kuwa wanaishi kwa kufauta
masharti ya wataalamu wa afya lakini pia kuachana  na dhana ya
kuambukiza magonjwa hayo kwa makusudi hasa kwa wale ambao bado hawana
maambukizi

mulongo aliyasema hayo wakati akiongea kwenye uzinduzi wa chanjo kwa
kina mama wajawazito mpango ambao unatekelezwa chini ya Shirika la
Egpaf

Alidai kuwa kwa sasa wapo baadhi ya wagonjwa ambao wanatumia mwanya
huo kuwajerui wale ambao hawana ugonjwa jambo ambalo sio jema kwenye
jamii

alifafanua kuwa wagonjwa hao wanapaswa kuhakikisha kuwa wanafuta
taratibu za wataalamu wa afya lakini pia wahakikishe kuwa kamwe
hawaongezi idadi ya wagonjwa zaidi

"jamani ni lazima tufike mahali tuwe na tabia ya uzalendo lakini pia
tuhakikishe kuwa tunajiengua kwa kusababisha mtikisiko kwenye taifa
kwa ajili ya makusudi tuawalinde wale ambao hawana na wala makusudi
kamwe hayawezi kutusaidia sisi bali yanachangia sana
kutuangamiza"aliongeza Mulongo

Naye mganga mkuu wa mkoa wa arusha Frida Mokiti alisema kuwa pamoja na
jitiada mbalimbali ambazo zinaendelea kufanyika lakini bado kasi ya
maambukizi kwa mkoa wa Arusha ipo juu sana.

Mokiti alifafanua kuwa mkoa umeweza kuweka mikakati mbalimbali ya
kupambana na ugonjwa huo ingawaje nao wagonjwa nao wanatakiwa
kuepukana na kusambaza kwa makusudi bali wanatakiwa kuchukua tahadhari
tena kwa haraka sana.

CCM WAWAFARIJI WAGONJWA

MWENYEKITI WA CCM TAIFA, JAKAYA KIKWETE

CHAMA  cha Mapinduzi Wilaya ya Karatu mkoa wa Arusha kimefanikiwa kutoa msaada kwa wagonjwa zaidi ya 100  wa hospitali teule ya wilaya ya Karatu(DDH KARATU)huku lengo likiwa ni kuwafariji na kuanza kutangaza mkakati mpya ambao utawasaidia wagonjwa kila mara .
akiongea na waandishi wa habari wilayani humo mara baada ya kukabidhi misaada hiyo Mwenyekiti wa Wilaya hiyo Bw Mustapha Mbwambo alisema kuwa misaada hiyo imetolewa kama njia mojawapo ya kutimiza upendo
Mustapha alisema kuwa kwa sasa wameweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa inawasadia wagonjwa na hata wale ambao hawajiwezi kwa misaada mbalimbali ambayo itaweza kuwasaida na kuona kuwa bado serikali na uongozi wa wilaya unawakumbuka.
'ilani ya chama chetu inasema kuwa tuwapenda na tuwajengee mazingira ya kupona wagonjwa sasa sisi hapa Karatu tumeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa kila mara tunatoa msaada lakini pia kuwafariji wagonjwa ambao hawana uwezo na zoezi hili halitakuwa kwenye maazimisho haya ya miaka 37 pekee"aliongeza Mustapha.

Katika hatua nyingine Katibu wa chama hicho ambaye ni Bi Elly Minja alisema kuwa kwa sasa Chama hicho kimeanza kutekeleza ilani ya Chama hicho lakini pia kuanzisha utaratibu maalumu wa kuweza kuwasaidia wananchi kwenye masuala ya msingi ambayo wakati mwingine yanachangia sana umaskini .
Alifafanua kuwa kwa mikakati ambayo inalenga kwenye masuala ya msingi yatachangia kwa kiwango kikubwa sana historia ya mji huo wa Karatu ambao kwa sasa bado unahitaji nguvu kubwa sana ya chama hicho.
"leo tumeweza kufanya mambo mbalimbali ya kichama lakini pia tumeweka malengo ya kuhamkikisha kuwa hata ilani ya chama inatekelezwa kwani kama ikifanikiwa basi itaweza kuwasaidia sana wananchi wa hapa kwetu na hivyo hata kwa mkoa wa arusha nako historia ikiwemo ya umaskini itabadilika sana"aliongeza Bi Minja.

Wakati huo huo akiongea na wananchi wa wilaya hiyo  kwenye viwanja vya Mazingira Bora Mgeni Rasmi kwenye maazimisho hayo, Daniel Awaki ambaye ni Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama hicho kwenye Wilaya hiyo ya Karatu alisema kuwa toka kuanzishwa kwa chama hicho miaka 37 iliyopitwa kuna mabadiliko makubwa sana na mabadiliko hayo hayapaswi kupuuzwa wala kuzomewa na mtu yeyoete.
"tujiulieze kwa sasa ukitoka Arusha mpaka hapa unatumia muda gani na hapo awali ilikuwaje, na wala sio kwenye sekta hiyo pekee bali hata kwenye sekta nyingine za msingi sasa mafanikio kama haya hatupaswi kuyapuuza hata kidogo"aliongeza Awaki.
mwisho

JAMBO SQURD WAFANYA KWELI ARUSHA

WASANII WA KUNDI LA JAMBO SQUARD


WASANII maarufu ambao wamefanikiwa kufanya vizuri katika soko la muziki wa kizazai kipya maarufu kama Jambo  Squard mwishoni mwa wiki walipagawisha vilivyo mashabiki wao katika uwanja wa sheikh Amri Abeid  jijini Arusha.

Wasanii hao ambao walisindikizwa na kundi zima la Balance Diet lililopo jijini hapa walipiga shoo ya kukata na shoka wakati kituo cha redio 5 kilichopo jijini Arusha kufungua mwaka na mashabiki wao kutoka mikoa ya Arusha,Kilimanjaro na Manyara.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa kituo hicho Robert Francis meneja mbunifu wa kampuni ya Tan Communication Media Vicky  Mwokoyo alisema kuwa wameamua kufanya tamasha hilo ili kuwawezesha mashabiki wa kituo hicho na mashabiki wa Jambo Squard kupata buradani katika viwanja hivyo ambayo kwa muda mrefu hawakuipata.

Hata hivyo alisema kuwa tamasha hilo ni kama kufungua mwaka na kurudisha burudani na mapenzi yao kwa mashabiki wao kama ambavyo mashabiki wamekuwa wasikilizaji bora   kituo hicho ambacho kwa sasa kimekuwa na kutanuka karibu mikoa yote ya Tanzania.

Mbali na hayo pia meneja huyo aliongeza kuwa  kwa mwaka huu 2014 watakuwa na matamasha mengi lengo likiwa ni kutoa burudani na kuwa na desturi ya kukutana na mashabiki wao ikiwa ni moja ya kufahamu vitu gani wanaihitaji zaidi lakini pia kuwawezesha mashabiki wote kupata burudani zaidi hata wale wa hali ya chini kwa kuweka viingilio ambavyo havitawanyima mashabiki wengine kukosa burudani

“tutakuwa tunafanya mara kwa mara matamasha kwa mwaka huu tumejipanga lengo ni kutoa burudani zaidi nakuwawezesha wote kushiriki hata wale wa mashabiki wetu wasiojiweza nao ni sehemu yetu na ni lazima wapate burudani”alisema Vicky

Mbali na wasanii hao wa Jambo Squard kupiga ambayo ama kwa  hakika mashabiki waliridhika wasanii wengine wengi walipata fursa ya kuonesha vipaji vyao kama Spark,na Kundi la balance Diet linaloundwa na vijana watatu.
Mwisho,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

MWEKEZAJI MERU AVAMIWA



ZAIDI ya wananchi 200 kutoka katika Kijiji cha Karangai Kata ya Mbuguni Wilyani Meru Mkoani Arusha wamevamia shamba la Mwekezaji wa kampuni ya Tanzania Plantation na kuharibu mazao, sanjari na kuchoma nyumba moto nyumba  kwa madai kuwa wanataka kumiliki ardhi yao.

Akiongelea suala hilo Meneja wa kampuni hiyo ya Tanzania Plantatio Andrew Slaa alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa nne za usiku ambapo wananchi walivamia makazi ya mwekezaji wao na kisha kuharibu mali ambazo thamani yake bado haijajulikana mpaka sasa.

Slaa alisema kuwa hataivyo wananchi hao walikuwa na silaha za jadi waliweza kutekeleza ahadi walizopewa na viongozi mbalimbali wa Kata hiyo akiwepo Diwani wa kata hiyo kuwa wanatakiwa kupewa ardhi yao.

"hivi karibuni wanasiasa walidai kuwa muwekezaji huyu ambaye anafanya kilimo katika mashamba haya hayupo kwa mujibu wa sheria kwaiyo hii ardhi ni mali yao na kutokana na kauli hiyo wananchi sasa juzi waliamua kuingilia kati na kisha kuharibu mali za huyu mwekezaji huku wakidai kuwa ardhi yote ambayo ni zaidi ya hekari 2000 ni mali yao"aliongeza Slaa

Alisema kuwa wao kama watendaji wakuu wa kampuni hiyo tayari wanamipango lakini hata mikakati ya kuhakikisha kuwa wanakuwa na ujirani mwema na wananchi lakini wananchi nao wanakiuka sheria za uwekezaji na kisha kusababisha hasara kubwa

Aidha kwa upande wa Mwekezaji mkuu wa kampuni hiyo Tanzania Plantation,Bw Pkadeep Lodhia alisema kuwa wananchi hao wamesababisha uharibifu mkubwa sana wa kuchoma nyumba , lakini pia kuharibu mbogamboga ambazo zilikuwa zimerpandwa kwa makusudi ndani ya eneo hilo

Alisema kuwa mara nyingi sana amekuwa akitishiwa maisha na wananchi hao ambao wakati mwingine humwambia kuwa amepora ardhi yao na hivyo hata kufikia uamuzi wa kutaka kumchoma yeye na gari lake jambo ambalo ni shinikizo kubwa la wanasiasa.

"mimi naogopa hata wakati mwingine kufanya kazi zangu ndani ya shamba hili kwani kuna saa ambazo nanusurika kufa kwa ajili ya wananchi wananitishia maisha lakini sio mimi tu hadi wafanyakazi wangu lakini mpaka sasa nimeshapata hasara kubwa sana ya Mamilionhi ya fedha kutokana na uharibifu huu wa mali"aliongeza Lodhia

Pia alisema kuwa anaiomba mamlaka husika kuhakikisha kuwa wanafanya uchunguzi wa kikamilifu zaidi yake na shamba lake lakini pia hata kuweza kuwachukulia sheria kali wanaosababisha uharibifu huo wa mara kwa mara kwani yeye ni mmiliki wa shamba hilo kuanzia mwaka 1995.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Munasa Nyirembe alisema kuwa Mwekezaji huyo yupo kwa mujibu wa sheria ya wawekezaji hapa nchini lakini wananchi nao wanapaswa kujua na kutambua kuwa wanachokifanya ni makosa tena makubwa na hivyo sheria itaanza kuchukua mkondo wake.

Naye Diwani wa kata hiyo ya Mbuguni,Thomas Mollel alisema kuwa kamwe hawezi kusiistiza uvamizi kwa mwekezaji huyo na kwa kusema hivyo anamuonea kwani sheria haiwezi kumruhusu kufanya hivyo.

DC ARUSHA AWATAKA WANANCHI KUTOPENDELEA KUWAPELEKA WANFUNZI NJE YA NCHI

MKUU WA WILAYA YA ARUSHA AKIAPA KUWATUMIKIA WANANCHI WA ARUSHA,PICHA NA MAKTABA YETU


NA ,MWANDISHI WETU, ARUSHA
Watanzania wametakiwa kuondokana na dhana ya kuwwapeleka watoto wao
nje ya nchi kwa ajili ya kuweza kupata elimu jambo ambalo hata kwa
shule za Tanzania wana uwezo huo wa kuboresha zaidi elimu

Asilimia kubwa ya watanzania wanadhani kuwa kumpleka mtoto au
mwanafunzi nje ya  nchi ndio kumjenga jambo ambalo halina hata ukweli
ndani yake

hayo yameelezw ana mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela kwa niaba ya
mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo wakati akiongea na umoja wa
wamiliki wa shule na vyuo binafsi kwa mkoa wa Arusha(TAMONGSCO) mapema
jana.

Mongela alisema kuwa dhana hiyo imeshapitwana wakati na hivyo wananchi
wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanaboresha shule zao na hivyo kuweza
kutoa fursa

Aisha alisema kuwa fedha ambazo wanazitumia nje ya nchi zingeweza
kusaidia baadhi ya shule katika michango na hivyo basi wanatakiwa kuwa
wazalendo

Amedai kuwa mzalendo wa nchi ni pamoja na kuhakikisha kuwa kwanza
unatoa vipaumbele kwa vitu ambavyo vipo ndani ya nchi lakini pia
unaweza kuvipenda

"pendeni sana shule za hapa tanzania kwani zipo baadhi ambazo kwa
kweli zinatoa elimu kwa wakati sana na zinafaa kuliko zile za nje ya
nchi, nakama mkiziboresha basi nanyi mtapata hata wanafunzi wenyewe
kutoka nje ya nchi na kwa hali hiyo mtakuwa mmenda sanjari na soko la
nchi za EAC'aliongeza Mongela

naye Mwenyekiti wa umoja huo Ester Lema alisema kuwa pamoja na kuwa
wana uwezo wa kuwasiaida wananchi kupunguza tatizo la kwenda nje ya
nchi lakini bado wanakabiliwa na changamoto nyingi

Ester alitaja changamoto ambazo wanakabiliana nazo kuwa ni pamoja na
kodi kubwa ambayo wanatozwa, lakini hata riba ambayo inatolewa na
asasi mbalimbali za kifedha.

KANISA LAAZISHA UTARATIBU WA KUOMBEA UCHAGUZI WA MWAKA 2015

Raisi Jakaya Kikwete



KANISA la T A G Patmo nkoanekoli lilopo Wilayani meru mkoani arusha limeweka mikakat mbalimbali ya kuombea uchaguzi wa taifa la  Tanzania ambao unatarajiwa kufanyika mapema mwakani 2015

Aidha uamuzi huo wa kufanya maombi ambayo yanafanyika kila mwanzo wa mwezi ili kuweza kuraishsisha uchaguzi huo wa wabunge pamoja na madiwani wa kata zote

 Akiongea kanisani hapo kwenye ibada ya siku ya jumapili ambayo iliongozwa na neno la mungu la kuwahimiza wakristo kutojiinua mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Japheti Nanyaro alisema kuwa utararibu huo utaweza kuwasaidia sana taifa

nanyaro alisema kuwa,maombi hayo ambayo yanafanywa na kanisa hilo yanalenga sehemu mbalimbali ambazo ni muhimu sana kwenye maisha ya kiroho ya mkristo wa sasa


alitaja kuwa wakati wa uchaguzi na kampeni mbalimbali za nchi panakuwa na roho lukuki za kishetani ambazo zinaibuka ambapo pia wakati mwingine roho hizo husababisha hata baadhi ya damu ambazo hazina hatia kuweza kuibuka na kufanya kazi

aliongeza kuwa mbali na roho hizo kuweza kuibuka lakini pia wakati mwingine kuna kuwa na maroho ya kuwanyima haki wanyonge hasa wale ambao wameitwa na Mungu kutokana na watu ambao wapo kuweza kutumia veo vyao kuiba haki


pia aliongeza kuwa nayo makanisa mengine yanatakiwa kuhakikisha kuwa yanaweka utaratibu wa kuweza kuomba juu ya matukio ya kitafia ndanui ya nchi kwani wakati mwingine roho za kujiinua nazo zinachangia sana hata wananchi kukosa haki zao za msingi

mbali na hayo pia aliwataka nao wakristo kuhakikisha kuwa wananchana na tabia ya kujiinua kutokana na vyeo vyao vya kanisa lakini hata vile vya kidunia kwani hali hiyo imesababisha walio wengi sana hasa wale wenye tabia hizo kuangamia bila kujijua

"nawasihi sana hakikisheni kuwa kamwe hamujiinui bali mnainuliwa na bwana mwenyewe ili msiweze kushuka ila mkjiinua na kutumia njia za mkato kwenye maisha au uongozi wa maisha yenu ya kila siku ni lazima mtapata shida na mtadhalilika sana subirini neema ya bwana iweze kukufika kwenye kila jambo"aliongeza Nanyaro

MWISHO