KITUO CHA UTAFITI WA MAZAO CHASHINDWA KUFIKISHA TEKNLOJIA 30
KWA WAKULIMA KWA UKOSEFU WA FEDHA
KITUO cha Utafiti wa mazao ya kilimo kanda ya
kaskazini(SARI) kimeshindwa kufilkisha teknolojia mpya thelathini kwa wakulima kwa zaidi ya miaka
minne mfululizo kutokana na kukabiliwa na uhaba wa Fedha hali ambayo inafanya
malengo mbalimbali ya Kilimo kwanza kufikiwa
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi mkuu wa Kituo hicho Dkt
Mboya Mgendi wakati akiongea na mkuu wa mkoa wa Arusha bw Magesa Mulongo ndani
ya viwanja vya Taso Nane Nane Mjini wakati alipotembelea banda la Kituo hicho
Dkt Mgendi alisema kuwa kwa Muda mrefu Serikali imekisahau
kituo hicho huku kituo hicho kikiwa ni moja ya vituo ambavyo vinahudumia Mikoa
ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro, na Tanga ambapo pia mikoa hiyo ni Mikoa ambayo
inaitaji msaada mkubwa sana
katika kuimarisha shuguli za kilimo hasa vijijini
Alisema kuwa hapo awali Kituo hicho kilikuwa ni moja ya
vituo ambavyo vilikuwa vinamsaidia sana mkulima hasa wa chini na wa kijijini na
matunda yake yaliweza kuonekana katika uzalishaji na ukulima tofauti na sasa
ambapo baadhi ya Vijiji vinashindwa kufikiwa kutokana na uhaba wa fedha ambao
umedumu katika kituo hicho kwa miaka minne sasa.
“tunasikitika sana kwa kuwa tuna buni teknolijia kila siku
tena teknolojia ambazo ni mpya kabisa kisha zinashindwa kuwafikia walengwa kwa
kuwa tunafikaje ni lazima fedha itumike kusafirisha hata hawa wataalamu, na
kutokana na hilo tunabaki na hizi teknolojia wakati walengwa wa hizi teknolojia
ni wananchi tena wa chini sasa Serikali
inatakiwa kuliangalia suala hili kwa undani sana ili kuweza kuboresha zaidi
Kilimo kwanza”alionngeza Dkt Mgendi.
Aidha Dkt Mgendi alisema kuwa kutokana na hali hiyo
imesababisha malengo mbalimbali ambayo yanakusudiwa na kituo hicho kushindwa
kufikiwa huku Serikali nayo ikilia na
kuweka Mikakati mbalimbali juu ya Kilimo kwanza hali ambayo kama ingetumika kwa
kuwawezesha wataalamu mbalimbali wa
kituo hicho basi Kilimo hasa kwa mikoa ya Kaskazini ingeboreka zaidi.
Pia aliiomba Serikali kuhakikisha kuwa inaangalia kwa undani
sana umuhimu wa kituo hicho hassa kwa Mikoa ya Kanda ya Kaskazini ambapo kuna
changamoto kubwa sana ya Matumizi sahihi ya
utafiti wa kilimo, Mbegu bora za
kilimo,pamoja na dhana ambazo bado wakulima wanaitaji elimu zaidi kutoka kwa
wataalamu hao wa kilimo bora.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha bw Magesa Mulongo alisema kuwa
Kituo hicho kina umuhimu mkubwa sana hasa kwenye Kilimo kwanza na Changamoto
mbalimbali ambazo zinaikabili kituo hicho zitasikilizwa ili kuendelea
kuimarisha zoezi zima la Kilimo kwanza hasa kwa Mkoa wa Arusha ambao bado
unaitaji sana nguvu ya watalaamu wa Kilimo bora
“Nitakuja katika kituo chenu cha utafiti tutaongea ili
tuweze kuona juu ya hili suala ambalo limeongelewa hapa ingawaje na kituo hiki
kinatakiwa kuhakikisha kuwa kila kitu ambacho wanakizalisha kinatakiwa kuwepo
kwenye mitaa yote ya kanda ya kaskazini ili kuboresha Kilimo kwanza ndani ya
Mikoa hiyo husika”aliongeza Bw Mulongo.
MWISHO
No comments:
Post a Comment