Thursday, April 26, 2012

WAJASIMALI 70 WA KKKT WAPATIWA MAFUNZO


Wajasiriamali wanawake zaidi ya 70 kutoka kanda ya kaskazini na kati ya dayosisi  za kanisa la kilutheri wamepatiwa mafunzo ya ujasiriamali ya siku nne yaliyolenga kuwajengea uwezo ufahamu, na elimu ya kujikomboa na umaskini.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo mkurugenzi wa mpango  wa kazi za wanawake na watoto kkkt makao makuu arusha Bi Rachel Ramadhani alisema kuwa licha ya changamoto zinazowakabili ikiwemo ya fedha lakini mafunzo hayo yatawatoa katika utegemezi na kuweza kujiendesha na kuandaa semina nyingine kama hizo. kwani wanawake wengi wameathiriwa na mfumo dume.

alisema bi ramadhani kuwa ukosefu wa elimu ya darasani na elimu ya mazingira kutokana na mfumo dume kumewaacha kinamama wakiwa hawana mtegemezi na kuishi kwenye lindi la umaskini na hili kanisa imeliona ndiyo maana likaanza kupigana na umaskini wa kinamama na vijana ilikuondokana na taifa tegemezi.

alisema bi Rachel kuwa dayosisi zaidi ya 7 zinashiriki  zikwemo dayosisi ya kaskazini,dayosisi ya Pare,dayosisi ya kaskazini kati,dayosisi za Mbulu,Meru,kaskazini mashariki,na kati na kuwataka wakinamama kufahamu kuwa kitu ulichonacho kiwe halali kitawafanya kuondokana na umaskini wa kujitakia hata mchicha ni biashara halali isiyohitaji fedha za kukopa kwenye asasi za kifedha unapatikana kwa njia ya kujituma na kujiamini aliongeza bi ramadhani

Kuwa wanachangamoto nyingi kubwa ni fedha lakini elimu hii itasaidia kuondokana na kuomba omba au kutafuta wafadhili wa kusaidia semina kama hizo na kuwataka angependa kuwaambia biashara si lelemama biashara ni nia na wazo lakujenga na ni kitu chochote halalikinachoweza kuuzika tufanye sasakwani tunamazingira yetu yanakila kitu cha kuweza kutusaidia.

Nae mjasiriamali aliyepata mafunzo hayo bi Elizabeth Ngoi alisema kuwa anamshukuru mama ramadhani kwani hapo mwanzo hakuwa anajua kuwa kunapato la kwanza na patozalishi linaloweza kumuendeleza mtu na kuondokana na lindi la umaskini na kuwa akifika nyumbani atakuwa balozi mzuri wa kuwafundisha wengine na kuwa atakuwa na uwezo wa kubuni biashara nyingi zaidi kutakana na mafunzo aliyopata.
MWISHO.

chanzo cha habari na Queen Lema,

0758907891

Arusha

CHONDE CHONDE ONGEZEKO LA VIJANA MANISPAA YA ARUSHA

MANISPAA YAKABILIWA NA ONGEZEKO LA VIJANA

Na queen lema, arusha

Manispaa ya mkoa wa arusha kwa sasa inakabiliwa na changamoto ya
ongezeko kubwa la vijana ambapo ongezeko hilo linasababishwa na baadhi
ya vijana wa vijijini kukimbilia mijini kwa ajili ya kutafuta ajira.

Hayo yamebainishwa jana na mkurugenzi wa taasisi ya maendeleo ya
vijana (YDN) Bw Elipokea Urio wakati alipokuwa akiongea na Majira
kuhusu mabadiliko ya maitaji ya vijana kwa mkoa wa arusha hususani
ndani ya halmashauri ya manispaa ya arusha

Bw Elipokea alibainisha kuwa ongezeko hilo ambalo limeongezeka kwa
kipindi cha miaka mitano sasa linasababishwa na matatizo mbalimbali
likiwemo tatizo la hali ngumu ya maisha hasa ya vijijini


Alisema kuwa mwaka 2002 vijana katika manispaa ya arusha kulikuwa na
vijana chini ya laki moja wakati kwa sasa kuna ongezeko kubwa sana la
vijana laki moja sabini elfu mia tano na hamsini na saba ambapo napo
nusu yao hawana ajira.

“tukijaribu kuangalia sana tunaweza kuona kuwa nusu ya hawa vijana
hawana ajira kutokana na matatizo na changamoto mbalimbali
ukilinganisha manispaa na jiji la arusha ni mji wa kitalii hivyo kuna
umuimu mkubwa wa serikali kuliangalia suala hili kwa undani”aliongeza
Bw Elipokea.

Katika hatua nyingine bw Elipokea alisema kuwa nusu ya vijana hao
ambao hawana ajira kwa sasa wamekosa  ajira kutokana na changamoto
mbalimbali  ambapo changamoto kubwa ni pamoja na vijana kushindwa
kutumia na kutambua fursa mbalimbali zilizomo kwenye ngazi ya
vijiji,kata,na halmashauri

Alisema kuwa kama vijana wa leo wataweza kutambua fursa mbalimbali
ambazo zimo kwenye ngazi hizo basi wataweza kunufaika hata kwa njia ya
mikopo  hali ambayo itaweza kuinua hata kiwango cha maisha.

“katika ngazi ya halmashauri unakuta kwa mfano fedha zimetengwa kwa
ajili ya vijana lakini fedha hizo vijana hawazitumii wala
hawazifuatlii kwa visingizio kuwa sio mali yao basi fedha hizo
zinaenda kwenye matumizi mengine sasa  kwa hali hiyo tatizo la uhaba wa ajira linazidi kuku asana katika jamii”aliongeza bw Elipokea.

Aliwataka vijana wa hususani katika manispaa ya arusha kuhakikisha
kuwa wanajijengea tabia ya kufuatilia fursa mbalimbali ambazo zimo
kwenye ngazi za serikali ikiwa ni pamoja na kutafuta mbinu ya
kujiajiri wao wenyewe ili kuepukana na tatizo la uhaba wa ajira.

MWISHO

chanzo cha habari na Queen Lema,Arusha

0758907891

Arusha

WATU MILION 45 HATARINI KUPATA MAGONJWA YASIYOPEWA KIPAUMBELE

JUMLA ya watu milioni 45 duniani hasa waishio katika jamii za kifugaji
wako katika hatari ya kupata magonjwa yasiyopewa kipaumbele kutokana
na kukithiri kwa changamoto mbalimbali ikiwemo uchafu wa mazingira, na
uhaba wa maji

 Juhudi za kuahakikisha kuwa magonjwa  hayo yanathibitiwa wilaya 75
kati ya wilaya zote nchini  tayari zimeshafikiwa na utekelezaji wa
ugawaji wa madawa  kwa mwaka 2011.

Hayo yalisemwa na mkurugenzi katika huduma za kinga kitengo cha
kutibiti magonjwa yasiyopewa kipaumbele  Dr Peter Mbuji wakati
akifungua  mkutano wa wizara ya afya na ustawi wa jamii uliofanyika
mjini hapa.

Alisema kuwa magonjwa yasiyopewa kipaumbele  ni pamoja na
matende,kichocho,usubi trakoma na minyoo ya tumbo ambapo haya  ni
magonjwa ambayo yalikuwepo toka awali na yako nchi nzima  lakini
tayari wizara inatoa dawa na mikakati imetumika ili kuhakikisha kuwa
yanatibiwa.

Alieleza kuwa mkakati na sera za wizara zipo za kuhakikisha kuwa
magonjwa hayo yanathibitiwa na moja ya  mikakati hiyo ni kuhakikisha
kuwa kila kijiji kinakuwa na huduma ya kutoa kinga dhidi ya kuthibiti
magonjwa  hayo.

Kwa upande wake mratibu wa kitaifa wa kuthibiti magonjwa yasiyopewa
kipaumbele kutoka wizara ya afya  Dkt. Upendo Mwingira alisema kuwa
ili  magonjwa hayo yaweze kuteketezwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa
maeneo yote ambayo yana magonjwa hayo yanafanyiwa usafi     kwa kuwa
ndio njia pekee ya kuthibiti.
Aidha alisema kuwa ni vema watu wa mazingira wakahakikisha kuwa elimu
ya usafi wa mazingira inawafikia wananchi ili kuweza kuthibiti
magonjwa hayo.

Pia amefafanua kuwa katika magonjwa hayo matano kila wilaya ina
maambukizi ya magonjwa mawili ambapo wilaya 75 zimeshapatiwa dawa
ambapo hadi ifikapo mwaka 2014 nchi nzima itanufaika na utekelezaji
huo.

Naye mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu( NIMR)dr
Mwele Malechela almesema kuwa taasisi hiyo ina mchango mkubwa kutokana
na juhudi zilizotokana nautafiti ili kutafuta majibu ya kuendesha
mipango kwa ufanisi zaidi.
Alisema kuwa mkutano huo utaangalia jinsi ya kuboresha sera na njia
mbali mbali za kutoa huduma kwa watu wenye ugonjwa wa matende .
mwisho


chanzo cha habari na Queen Lema

0758907891

Arusha
SAKATA la wachungaji wa kanisa la sabato na uongozi wa kanisa hilo umechukua sura mpya mara baada ya wachungaji watatu ambao walikuwa wanashitakiwa kwa makosa ya kudaiwa kurudufu vitabu,kusema kuwa wanatoa muda kwa kanisa hilo kuomba radhi hata kwenye vyomboi vya habari na endapo kama watashindwa kufanya hivyo basi watawapeleka mahakamani.

Akiongea na mjini upako wa habari za ufalme wa mungu  kwa niaba ya wachungaji wengine wawili Dkt Tulla Paul alisema kuwa wameamua kufikia uamuzi huo kwa kuwa Kanisa hilo limepotosha umma na pia wameshindwa kufika hata kituo cha polisi ambapo ndipo waliposhitaki

Dkt Tulla alisema kuwa kwa mara ya tatu tena mfululizo Walalkamikaji ambao ni kanisa hilo wameshindwa kufika katika kituo cha kati cha polisi mjini hapa hali ambayo inafanya hata kesi hiyo ishindwe kupelekwa mahakamani

Alifafanua kuwa kanisa hilo la Sabato ambalo lilisema kuwa lina ushahidi dhidi ya wachungaji hao kurudufu vitabu vya nabii Hellen .G. White ni uongo kwa kuwa kanisa ndilo lilorudufu vitabu

“kanisa la Sabato ndilo lilorudufu vitabu na ushaidi upo kwa maana hiyo basi ni vyema tukaenda mahakamani tukapambane huko huko ila kama hawataki waombe radhi hadharani kwa kuwa wametuweka katika wakati mgumu sana na ni sawa na kifungo cha Nje kwa kuwa mara nyingi sana tunahudhuria kituoni ili kesi iende mahakamani lakini wao hawaji “aliongeza Dkt Tulla

Katika hatua nyingine alisema kuwa tukio hilo ni sawa na uonevu mkubwa sana na hata taasisi nyingine za dini nazo zinatakiwa kujifunza kitu kwa kuwa wamepoteza muda na rasilimali fedha kwa ajili ya madai ambayo si ya msingi

Walifafanua kuwa kwa muda wa zaidi ya Miezi mitatu sasa wamefuatilia kesi hiyo ambayo ni AR/IR/1130/2012 huku shuguli zao za kueneza injili nayo ikikwama hali ambayo ni kichocheo kikubwa sana cha kukata tama

“sasa kama sisi wengine tunatoka Mwanza tunakuja kwa ajili ya kesi ambayo tulifunguliwa sisi kwa kisa kuwa tumerudufu vitabu wakati ni uongo na walalamikaji hawaji ili kesi iende mahakamani basi huu si ni uongo wa ajabu sana jamani nini nafasi ya kanisa hapa na je mtu ambaye haamini anajifunza nini kutoka kwa hawa viongozi wa kanisa ‘alisema Dkt Tulla

 

chanzo cha habari na queen Lema

0758907891

 Arusha