Tuesday, February 28, 2012

MANABII MSIGEUZE HUDUMA HIYO YA UNABII KAMA BIASHARA- ASKOFU YONA


Manabii mbalimbali hapa nchini wameshauriwa kuhakikisha kuwa wanatumia karama hiyo vema ikiwa ni pamoja na kuacha kutumia karama hiyo kama kipato mojawapo cha kuweza kupata fedha.

Endapo kama watategemea kumtabiria mtu kitu na kisha kudai fedha ni wazi kuwa watakuwa wanafanya huduma hiyo kwa maslahi yao na  wala sio kwa maslahi ya Mungu ambayo wameitiwa.

Kauli hiyo imetolewa mjini hapa na Askofu Yona Suleman kutoka  Singida wakati alipokuwa akitoa neno katika kanisa la  all National  for Christian centre lilopo katika maeneo ya Jakaranda ndani ya manispaa ya Arusha, ambapo pia huduma hiyo ilienda sanjari na usimikwaji wa Viongozi mbalimbali katika kanisa hilo.

Aidha alisema kuwa hduuma ya utabiri sio mbaya kwa kuwa hata pindi Bwana yesu alipokuwa hapa duniani aliweza kufanya tabiri mbalimbali ambazo zilikwenda sambamba na uponyaji lakini hakudai fidia yoyote ile.

Aliongeza kuwa ili huduma yoyote ile iweze kukua ni lazima iende sambamba na utabiri na unabii lakini unabii huo pia uwe ni bure na ambao unalenga kuimarisha zaidi maisha ya mwanadamu ambaye ndiye anayetegemea Kanisa katika maisha yake.

"wapo baadhi ya watu na mimi nimeshawaona kabisa wanatoa unabii kwa mtu kisha wanadai malipo sasa hali hiyo ni mbaya sana kwa kuwa wanafanya hata kiwango cha imani za watu kushindwa kukua kwa kiwango ambacho kinaitajika"alisema Bw Yona.

Pia aliongeza kuwa na wale ambao wanapewa unabii juu ya mambo mbalimbali wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanapokea unabii huo vema ambapo pia mara baada ya kupokea unabii huo wanapswa kufanya toba

Alisisitiza kama toba hazitafanyika tena kwa wakati ni wazi kuwa wakristo hao watakuwa wanahama hama makanisa kwa ajili ya kutafuta Miujiza ambayo inatolewa na manabii hao wakati Mungu anapatikana mahala popote pale.

MWISHO                         

CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA

0758907891

ARUSHA 

No comments:

Post a Comment