Sunday, January 1, 2012

WALAZIMIKA KUKIMBIA MAKAZI KISA SALA, NA TOHARA, MORANI WAHARIBU KANISA


Familia tano zenye watoto zaidi ya ishirini zimelazimika kukimbia makazi yao ya kudumu kwa kipindi cha wiki tano sasa kwa kuhofia kutembezwa uchi na kupigwa na vijana wa kabila la kimasai”Morani”mara baaada ya kufanya ibada sanjari na kufanya tohara kwa njia za kisasa zaidi.

Familia hizo zimelazamika kufanya hivyo kwa kuhofia maisha yao pamoja na maisha ya watoto wao ambapo kundi kubwa la vijana wa kimasai wanawatafuta kwa makosa ya kuharibu na kuvunja mila zao kwa njia ya Sala pamoja na Kufanya tohara Mahospitalini.

Hayo yametokea katika eneo la Oljoro Mkoani hapa ambapo kwa muda wa wiki tano familia hizo zimelazimika kukimbia makazi yao kwa kuhofia kutembezwa mitaani Uchi, pamoja na kupigwa kipigo kikali.

Akiongea na “Upako wa habari za ufalme”mmoja wa wanafamilia waliolazimika kukimbia nyumba zao kwa hofu ya kutembezwa mitaani Uchi Bw Korduni Wilson, alisema kuwa Morani hao wamekuwa wakifanya vibaya sana kwa kuwa mila wanazozitaka zina madhara sana.

Bw Korduni alieleza kuwa wameamua kufikia uamuzi huo wa kukimbia nyumba zao kwa kuwa wao tayari wameshajua na kufahamu madhara ya kufanya tohara kwa njia ya kienyeji sanjari na kuabudu mila ambazo Morani hao wanazitaka.

“kati ya hizi familia tano nyinginezo hazijakimbia kwa kuwa wamefanya tohara kwa watoto wao bali Morani hao wamekuwa wakidai kuwa wanaharibiwa mambo ya Kimila hasa pale wanaposali kwa maana hiyo wanakataa hata makanisa kwa kuhofia Matambiko, na Mila”aliongeza Bw Korduni.

Pia aliongeza kuwa mara baada ya Morani hao kuona kuwa Kanisa linakubali na kusisitiza waumini wake kufanya Tohara kwa njia ya kisasa sanjari na kukataa Mila ambazo zina madhara kwa Mtanzania Morani hao waliktaa amri hiyo na kuvunja Kanisa la T.A.G  oljoro hali ambayo ilisababisha hasara kubwa sana.

Katika hatua nyingine Msimamizi  na Muangalizi  wa makanisa ya T.A.G mkoani hapa Bw Simion Vomo alisema kuwa wao kama kanisa hawataweza kuwasikiliza Morani hao kwa kuwa madai yao hayana Msingi Kisheria.

Aliongeza kuwa Kanisa litalazimika kuchukua hatua kali na za kisheria,kwa kuwa Morani hao wanasababisha amani ndani ya miji na Maboma ya wananchi kukosekana hali ambayo kama haitaweza kuchukuliwa tahadhari basi itazaa matatizo makubwa sana katika jamii.

Awali Kaimu Kamanda wa  Polisi mkoa wa Arusha Bw Akili Mpwapwa alisema kuwa bado polisi wanaendelea na Upelelezi,hivyo familia hizo tano ambazo zimelazimika kukimbia makazi yao kwa kuwahofia Morani hao, wanatakiwa kutoa Taarifa ili Sheria ichukue mkondo wake kwa kuwa wanachokifanya Morani hao ni Makosa.

MWISHO
 
CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA

ARUSHA 

0758907891.

No comments:

Post a Comment